SAKATA LA MHE LEMA KUBAGULIWA JANA MSIBANI LATUA BUNGENI
Wabunge
wawili wa Chadema, Peter Msigwa wa Iringa Mjini na Godbless Lema wa Arusha
Mjini wameomba mwongozo wa Spika kuhusu ubaguzi wa kisiasa uliotokea kwenye
msiba mjini Arusha Jumatatu.
Jana
Jumatatu jijini Arusha ilikuwa inaagwa
miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent
waliopoteza maisha katika ajali ya gari.
Wa
kwanza kusimana alikuwa Msigwa ambaye amehoji kama ni haki kutowapa fursa Meya
wa Arusha, Calist Lazaro na Mbunge wa jimbo hilo, Lema kutoa salamu za
rambirambi.
Lema
kwa upande wake amesema hata magari mawili ya kubeba wagonjwa yaliyotolewa na
yeye na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari yaliondolewa kwa sababu yana
majina yao.
Amesema
ni kwa sababu walimheshimu makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, vinginevyo mambo
kama hayo huwa hayatokei mbele yao.
Mwenyekiti
wa Bunge Najma Giga amesema atatoa
mwongozo huo baadaye.
No comments