RC GAMBO: TUTAWADHIBITI WOTE WANAOINGIZA SIASA MISIBANI
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjoTRTAiAhyYEqiRwT5l75kdH5CPbGVGUlqyNBc2ObKDlwk5HpnZCb1ril0Ul1qJy_v15KjaQ3fOdFsteh3Wyn45BQP5LbmMbTBpOdjcjWD7XFlzsANSf6HlVXzcatSS7esPhjWvhV1JKMv/s1600/1.jpg)
Mkuu
wa Arusha Mrisho Gambo amesema serikali itaendelea kuwathibiti watu wote
watakaotaka kuingiza siasa kwenye majanga mbalimbali hasa la vifo vya wanafunzi
wa Lucky Vicent na kuwataka watu kufuata utaratibu na maelekezo yanayotolewa na
serikali.
Mkuu
wa mkoa huyo alisema hayo jana wakati anapokea misaada inayoendelea kutolewa na
wadau mbalimbali na kuwataka wananchi na taasisi zinazoendelea kutoa rambirambi
kwa familia za wanafunzi waliofariki kufuata taratibu zilizowekwa ili kuepusha
migongano isiyo ya lazima.
Mbali
na hilo Gambo alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuwadhibiti wote watakaotaka
kuingiza siasa kwenye majanga likiwemo la vifo vya wanafunzi na amesisitiza
umuhimu wa kila mmoja kufuata sheria, taratibu na maelekezo yanayotolewa na
serikali.
No comments