MKURUGENZI WA HALOTEL AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UHUJUMU UCHUMI
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Viattel Tanzania (Halotel) Do Manh Hong, amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka saba likiwemo la uhujumu uchumi.
Mshtakiwa
Do Manh Hong amefikishwa mahakamani hapo na kuunganishwa na washtakiwa wengine
saba waliofikishwa mahakamani hapo mapema Mwaka huu.
Wote
kwa pamoja wanakabiliwa ma mashtaka kumi, kula njama. Kisimika mitambo ya
mawasiliano bila kibali cha TCRA, kutoa nyaraka za uongo, kusababisha hasara
kwa serikali ya Tanzania, ya milioni
459, kutumia mitambo ya mawasilino ambayo haijathibitishwa na namba za simu.
Mbali
na Hong, washtakiwa wengine ni Dilshad Ahmed (36), Rohail Yaqoob(47), Khalid
Mahmood (59), Ashfaq Ahmad (38), Muhamad Aneess(48), Imtiaz Ammar (33) wote
raia wa Pakistan na Ramesh Kandasamy (36) raia wa Sri-Lanka.
Kabla
ya kusoma kwa mashtaka, wakili wa Serikali, Jehovanea Zacharias aliiomba
mahakama kumuunganisha mshtakiwa Hong na kuwasomea washtakiwa wote makosa yao.
Imedaiwa
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa mshtakiwa Ahmed,
Yaqoob, Mahamood, Ahmad, Anees,
Kandasamy na Qammar Novemba 2016 Dar es Salaam walikula njama ya kutumia vifaa
vya mtandao.
Imedaiwa
kuwa, watuhumiwa walitengeneza mfumo wa kutumia huduma za mtandao kwa lengo la
kukwepa kodi ya kupokea na kusambaza
simu za kimataifa bila kibali cha TCRA.
Aidha
imedaiwa kuwa Novemba 20, 2016 waliingiza vifaa vya kielektroniki bila ya kuwa na leseni na kuvisimika bila ya kuwa na kibali cha TCRA.
Imedaiwa,
washtakiwa waliunganisha vifaa hivyo na
huduma za mitandao kwa lengo la kupokea na kusambaza mawasiliano bila ya
kuthibitishwa na TCRA.
Kwa
upande wa Kampuni ya Viettel Tanzania Limited na Do Hong wanadaiwa kati ya
Novemba 2016 na Februari 2017 maeneo ya ofisi za Halotel Victoria Kinondoni
walishindwa kuthibitisha taarifa iliyotolewa na Unex Company Ltd kwa lengo la
kusajili laini za simu 1000.
Kwa
upande wa washtakiwa Ahmed na wenzake sita wanadaiwa kuwa Januari 5 ,2016
walitoa Cheti chakughushi cha usajili wa kodi chenye namba 100-864-210
kuonyesha imetolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania wakati si kweli.
Mbali
na mashtala hayo, watuhumiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuisababisha hasara TCRA
na serikali ya Tanzania kiasi cha milioni 459.
Hata
hivyo, washtakiwa wote hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa
kuwa mshtaka yanayowakabili yako nchini ya sheria ya uhujumu uchumi.
Kesi
hiyo imeahirishwa hadi Machi 29,2017.
No comments