ZITTO KABWE: NINA WASIWASI NA UWEZO WA WAWAKILISHI WA ‘EALA’ KUTOKA CHADEMA
Mbunge
wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa
amesikitishwa sana na matokeo ya uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA)
uliofanyika jana usiku bungeni mjini Dodoma kwa upande wa Chadema.
Kupitia
ukurasa wake wa Facebook Zitto ameandika kuwa kuchagua watu bila kuangalia
uwezo, uzoefu na uhusika wao kulingana na sehemu wanapotakiwa kuwepo ni
kuliangamiza taifa, hasa ukizingatia changamoto zilizopo katika nchi hizo
Afrika Masahriki.
Amesema
kuwa nchi kama Rwanda, Burundi na Uganda zimepeleka wawakilishi mashuhuri na
wenye uzoefu mkubwa katika bunge hilo kulingana na umuhimu wa shughuli
zinazofanywa na bunge hilo.
“Jana
usiku nilikuwa na hasira sana, kufuatia matokeo ya uchaguzi wa wawakilishi wa
Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki (EALA) haiwezekani kuchagua wabunge
ambao hawana uwezo wa kwenda kujenga hoja, huku tukitegemea kupambana na
changamoto za muungano wa nchi hizi za Afrika Mashariki”ameandika Zitto katika
ukurasa wake wa Facebook.
Zitto Kabwe
8 hours ago
Jana usiku nilikuwa nimekwazika kufuatia matokeo ya uchaguzi wa wawakilishi wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki ( EALA ). Kufuatia hasira hiyo nikaandika kuwa wakati mwengine unajiuliza Kama unastahili kuwa kwenye nchi ambayo umo Kama raia.
Haikuwa sahihi Kabisa Kwa Kiongozi wa ngazi yangu kujutia uraia wangu kwa sababu tu ya kundi la watu wachache kuamua kuchagua wawakilishi wetu kwenye taasisi za kimataifa bila kujali uwezo, uzoefu na weledi wa wawakilishi husika....
See more
No comments