MHE LEMA ALAANI UBAGUZI ALIOFANYIWA MSIBANI ARUSHA
Mbunge
wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Godbless Lema ametoa
masikitiko yake na kuonyesha kuumizwa na kitendo alichofanyiwa jana wakati wa kuaga miili ya wanafunzi,
walimu na dereva waliofariki katika ajali ya basi.
Lema
anasema kitendo cha yeye kama Mbunge wa Arusha mjini pamoja na Meya wa jiji
kunyimwa nafasi japo ya kutoa pole kwa familia na wafiwa wakati wa kuaga miili
hiyo ni ubaguzi mkubwa.
==>Huu
ni Ujumbe wa Godbless Lema
Leo(jana)
katika msiba wa kuaga Wanafunzi waliofariki ktk ajali . Mimi kama Mbunge
mwenyeji niliyefiwa Jimboni kwangu pamoja na Mayor tulihudhuria maombolezo
hayo, ilikuwa ni itifaki ya kawaida kabisa kuelewa kuwa Mbunge pamoja na Mayor
watapaswa kutoa salamu za rambi rambi au kuwashukuru wageni waliofika kwa ajili
ya kutupa pole .
Nilisikia
toka jana jioni kuwa katika maombolezo haya leo kuwa Viongozi wa Chadema
watapaswa kutokuongea , nilimpigia simu Mbunge wa Ngorongoro Mh Ole Nasha ,
nikamweleza ubaguzi mchafu unavyopangwa katika jambo hili muhimu la kuaga
watoto wetu, alinihakikishia kuwa Makamu wa Rais asingeweza kukubaliana na
ujinga huu.
Kwenye
ratiba nilipoingia uwanjani , jina langu lilikuwepo kwenye ratiba kwa ajili ya
salamu za rambirambi, lakini baada ya Mkuu wa Mkoa kukabidhiwa itifaki, mambo
yalibadilika na ilionekana dhahiri kuwa sitakiwi kabisa kutoa pole kwa watu wa
jimbo langu waliofikwa na msiba huu mbaya. M/kiti Mbowe aliandika meseji kwenda
kwa M/ Rais kukumbusha umuhimu wa wenyeji kutoa salamu , Makamu wa Rais baada
ya kupokea meseji hiyo, alimwita Mkuu wa Mkoa , ndipo ilionekana kama kuna
ushindani unatokea kati yao , lakini hatukuweza kabisa kupata nafasi ya kutoa
salamu kwa wapendwa wetu.
Wabunge
wa CCM waliokuwepo ambao ni mawaziri wote waliweza kutoa pole ,huu ni ubaguzi
uliojaa ujinga na chuki mbaya kisiasa, nitaeleza madhara yake kwenye hotuba
yangu kesho , lakini nafikiri watoto mara nyingi huwa wanafuata
walichofundishwa na wazazi , pengine ingekuwa ni usaliti Mbunge Lema kusalimia
na kuwapa pole watu wake mbele ya Makamu wa Rais. Ni wazi sasa kwamba tofauti
yetu sisi kama nchi na Syria ni wakati.
Nawashukuru
wote waliotukimbilia kwa matatizo yaliyotokea Arusha, Mungu awabariki sana.
Msiogope , Mungu hadhiakiwi apandacho mtu ndicho avunacho
LEMA
No comments