HAYA NDIO MAAMUZI YA KAMATI YA MAADILI BAADA YA MHE MAKONDA KUKUTWA NA KOSA LA KUINGILIA UHURU WA BUNGE
Kamati
ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge la Tanzania, leo imewasilisha bungeni
taarifa za matukio mbalimbali ambazo imezifanyika kazi ikiwa ni pamoja na
kuwaita na kuwahoji wahusika kwa kukiuka kanuni za bunge nje na ndani ya bunge
hilo.
Miongoni
mwa taarifa hizo ni pamoja na ile ya kuingilia uhuru wa bunge kosa lililofanywa
na Paul Christian Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka bungeni, viongozi hao wate wawili wamesamehewa
kutokana na kukiri makosa yao na kuliomba radhi bunge la Tanzania.
Aidha,
Kamati ya Maadili ya Bunge imemsamehe Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman
Mbowe baada ya kukiri kutoa lugha ya kudharau mamlaka ya bunge.
Pia
Kamati ya Maadili ya Bunge imemuadhibu Mbunge Halima Mdee kutohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti
vilivyosalia kwa kudharau mamlaka ya bunge.
Hata
hivyo, Bunge limeazimia kumsamehe mbunge huyo
baada ya Wabunge wa pande zote kumuombea msamaha .
Katika
hatua nyingine,Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya amepewa karipio kali na
Kamati ya Maadili ya Bunge kwa kosa la kudharau Mamlaka ya Spika wa Bunge.
No comments