WAZIRI KAIRUKI: SERIKALI HAITAMVUMILIA MTUMISHI MWENYE CHETI FEKI

Inakadiliwa
kuwa watumishi 4,300 wapya wanataajiriwa kuajiriwa katika kada ya elimu na
wasanifu wa maabara ambapo ajira hizo mpya zinakuja bada ya kukamilika kwa
zoezi zima la kuhakiki watumishi hewa.
Hayo
yamebainishwa mkoani Tabora na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
Mh. Angela Kairuki, wakati akizungumza na watumishi na wanachuo, ambapo amesema
kuwa, kwa muda mwingi taifa limekuwa likikabiliwa na changamoto ya watumishi
hewa huku likipoteza fedha nyingi.
Aidha
Mhe. Kairuki amesema kuwa kamwe serikali haitamvumilia mtumishi ambaye
atabainika kuwa na vyeti feki, huku akiwataka watanzania kutambua madhara ya
vyeti hivyo kuwa ni kutopatikana kwa huduma stahiki huku akiwataka wahitimu
katika kada mbali mbali kutowaonea haya watu ambao wanataka kupora ajira za
wenzao.
No comments