LIPUMBA: KUNA NJAMA ZINAPANGWA ILI CUF IFUTWE
Mwenyekiti
wa chama cha wananchi CUF anayetambulika na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa
nchini Prof. Ibrahim Lipumba amesema ameandika barua maalumu kwa jukwaa la
wahariri kuonesha kusikitishwa kwake na vurugu zilizotokea hivi karibuni katika
mkutano wa CUF na kusababisha waandishi kufanyiwa fujo.
Prof
Lipumba ameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ameyasema
hayo katika mahojiano na mwandishi wa habari wa Azam Two na pamoja na mambo
mengine amemtaka katibu mkuu wa CUF Maalim Seif wakae wazungumze ili wamalize
tofauti zao na wakae wakijenge chama..
“Baada
ya kulisikia hilo niliamua kuchukua jukumu la kuwaandikia Jukwaa la wahariri
barua ambayo ipo mbioni kwenda kwenye ofisi zao kwamba mimi binafsi kama
mwenyekiti wa CUF nalaani kitendo cha kupigwa kwa waandishi wa habari na ni jambo
ambalo hatulikubali kabisa, hatuwezi kujenga Demokrasia ikiwa waandishi wa
habari hawafanyi kazi yao katika hali ya amani na utulivu”.
“Vile
vile kijana wetu amekatwa kisigino kwa panga na anavyo elewa yeye kijana
aliyemkata anaitwa Mohamedi Mgonvi na taarifa hii imepelekwa kwenye vyombo vya
dola kwa hiyo vyombo vya dola vinalishughulikia na tulitoa wito ambao ulitolewa
na Mkurugenzi wetu wa habari na uenezi”
“Mimi
toka awali nimeeleza kwamba nataka tumalize tofauti za kisiasa kwa mazungumzo
tupate suluhu tuheshimu katika ya chama chetu na nimekuwa nikimuita Maalim Seif
aje ofisi bugurudi aweze kuzungumza afanye kazi zake kama katibu mkuu na mimi
nimemfahamu Maalim Seif mwaka 1973 tukiwa wanafunzi wa chuo kikuu Dar es Salaam
kwahiyo hatuna sababu ya sisi kuwa na mgogoro huu na kuuruhusu kuendelea”
“Hivi
sasa kupitia taarifa zetu za kiuchunguzi zinaonesha kwamba kuna mbinu ya kutaka
chama hiki kiweze kufutwa kwa hiyo kuna matukio yanapangwa nje ya chama ili
paweze kutokea vurugu na zikishatokea waseme chama hiki hakifai kuendelea kuwa
chama cha siasa na utakuta kuna vyama vingine vya siasa vinashabikia na kutoa
wito ili chama hiki kiweze kufutwa” Prof. Lipumba
No comments