KAULI YA MBUNGE LIJUAKALI BAADA YA KUACHIWA HURU NA MAHAKAMA
Mbunge
Wa Kilombero Kupitia Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (Chadema) Mhe. Peter
Lijualikali Jana Amefanikiwa Kuachiwa Huru Na Maafisa Wa Gereza La Ukonga Baada
Ya Kukamilisha Taratibu Za Kutoka Gerezani.
Akizungumza
Mara Baada Ya Kutoka Gerezani Mbunge Lijualikali Aliwataka Watanzania Kutumia
Demokrasia Ya Kweli Katika Kutafuta Majawabu Ya Matatizo Waliyonayo Ili
Kubadili Taswira Ya Tanzania Na Kuwa
Nchi Ya Maendeleo Na Kuongeza Mshikamano Bila Kubaguana.
Kwa
Upande Wake Baba Mzazi Wa Mbunge Huyo Amberose Lijualikali Aliviomba Vyombo Vya
Dola Nchini Kufuata Sheria Za Nchi Zinavyoelekeza Katika Kutoa Maamuzi.
Kwa
Upande Wake Waziri Mkuu Mstaafu Na Mwenyekiti Wa Chadema Kanda Ya Pwani Mhe.
Fredrick Sumaye Aliyekuwepo Katika Gereza La Ukonga Dar Es Salaam Wakati Mbunge
Huyo Akiachiwa, Aliwataka Viongozi Na Watanzania Kutumia Demokrasia Katika
Kudai Haki Zao Ili Kulinda Amani Ya Nchi Iliyopo.
Hukumu
Ya Lijualikali Ilitenguliwa Jana Na Mahakama Kuu Baada Ya Kukaa Gerezani Kwa
Zaidi Ya Siku 70 Akituhumiwa Kufanya Vurugu Katika Uchaguzi Wa Mwaka 2015.
Katika Hukumu Hiyo, Lijualikali Alihukumiwa Bila Kupewa Masharti Ya Faini.
No comments