MAHAKAMA NCHINI KENYA YATOA AMRI ZUIO KWA MADAKTARI WA TANZANIA
Mahakama
ya Kazi nchini Kenya imeweka zuio la muda dhidi ya serikali ya nchi hiyo
kuajiri madaktari kutoka nje ya nchi hiyo.
Jaji
Nelson Abuodha wa Mahakama hiyo ametoa amri hiyo baada ya Madaktari watano wa
Kenya kufungua malalamiko ya kuitaka serikali kusitisha mpango wake wa kuajiri
madaktari 500 kutoka Tanzania wakidai kuna madaktari wengi nchini humo ambao
hawajaajiriwa.
Madaktari
hao wameitaka Mahakama itoe amri inayoitaka serikali kuajiri madaktari 1,400
ambao hawana ajira ambao wamefuzu katika taaluma ya utabibu na iizuie serikali
kuacha kabisa kuajiri madaktari na wataalam wengine wa afya kutoka nje.
Hatua
hiyo imekuja baada ya Rais Magufuli kukubali ombi lilitolewa na Rais Uhuru wa
kuipatia Kenya madaktari katika kusaidia utoaji tiba baada ya kutokea kwa mgomo
wa madaktari nchini humo wenye lengo la kushindikiza waboreshwe maslahi yao.
No comments