KAMPUNI YA BIA (TBL) YAWAFUTA KAZI WAFANYAKAZI 100 NDANI YA SAA 24
Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries (TBL),
imepunguza watumishi wake takribani 100 ndani ya saa 24.
Kwa
mujibu wa taatifa toka kwa watumishi wa
TBL, watumishi waliopunguzwa ni wale wa
kitengo cha masoko.
Mtoa
taarifa mmoja kutoka kwenye duru za uongozi wa TBL ambaye hakutaka jina lake
litajwe, alisema kuwa uamuzi huo ulitekelezwa Jumatatu ya wiki hii.
Alisema
sababu kuu ya kupunguza wafanyakazi hao ni kulinda uchumi wa kampuni baada ya
mauzo ya bidhaa kuporomoka kwa kasi katika kipindi cha mwaka jana hadi mwaka
huu.
Ofisa
masoko mmoja wa kampuni hiyo ambaye hajakumbwa na panga la kupunguzwa kazi,
alidokeza kwamba uamuzi huo unatokana na hali ya mauzo na uchumi wa kampuni
kutokuwa rafiki.
Aliongeza
kuwa uamuzi wa Serikali wa kuzuia biashara ya pombe kali zinazofungashwa kwenye
mifuko ya plastiki(viroba) umeathiri kwa kiasi kikubwa soko la bidhaa yao aina
ya Konyagi.
“
Wameachishwa kinyama sana, waliitwa siku ya Jumatatu na kuachishwa papo hapo(on
spot), wakaambiwa wayaache magari yao na kusaini fomu ya kuondoka, miye kwa
bahati nzuri nimepona. Na hili jambo la
viroba ndio limepigilia msumali wa mwisho,” alisema ofisa huyo.
Msemaji
wa Kampuni ya TBL, Georgia Mutagahwa alipotafutwa kwa ajili ya uthibitisho wa
taarifa hiyo, hakupokea simu kila ilipopigiwa.
Credit:
Mtanzania
No comments