HII HAPA KAULI YA ASKOFU NKOLA NA WACHUNGAJI BAADA YA KUFUKUZWA KAZI KANISA LA AICT

Askofu
mkuu wa kanisa la AICT Silas Kezakubi akitangaza uamuzi wa kuwachukulia hatua
viongozi watano wa kanisa hilo.

Aliyekuwa
askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Dkt. John Kanoni Nkola
akizungumza na Malunde1 blog kanisani baada ya askofu mkuu wa kanisa hilo
kutangaza kuwachukulia hatua viongozi watano wa kanisa hilo akiwemo askofu
Nkola

Aliyekuwa
katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi
ya Shinyanga Jakobo Mapambano ambaye ni miongoni wa wachungaji waliovuliwa
uchungaji akizungumza na waandishi wa habari

Waliokuwa
wachungaji wa kanisa la AICT,Jakobo Mapambano(kushoto) na Dkt. Meshack Kulwa(
kulia) wakimsikiliza askofu mkuu wa kanisa la AICT Silas Kezakubi akitangaza
uamuzi uliochukuliwa na kanisa kuwawajibisha viongozi wa tano wa kanisa hilo
*************
Kanisa
la African Inland Church Tanzania (AICT) limemstaafisha askofu wa kanisa la
AICT Dayosisi ya Shinyanga Dkt. John Kanoni Nkola na kumtaka kujiuzulu nafasi
ya uaskofu askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Mwanza John Bunangwa kwa
kushindwa kusimamia vizuri fedha za kanisa kwa ajili ya kuendesha shule ya
sekondari Bishop Nkola iliyopo mjini Shinyanga.
Mbali
na maaskofu hao kuchukuliwa hatua,pia wachungaji watatu wa kanisa hilo
wamevuliwa nafasi ya uchungaji ambao ni Emmanuel Isaya,Dkt. Meshack Kulwa na
Jakobo Mapambano aliyekuwa katibu mkuu wa kanisa hilo dayosisi ya Shinyanga.
Akitoa
taarifa kwa waumini wa kanisa la AICT
Kambarage mjini Shinyanga wakati wa ibada ya Jumapili,Askofu mkuu wa kanisa la
AICT nchini Tanzania askofu Silas
Kezakubi alisema maamuzi ya kuwachukulia hatua viongozi hao yametokana na kikao
cha baraza la utendaji la sinodi kuu AICT.
Askofu
Kezakubi alisema viongozi hao wamelitia aibu kanisa kwa kushindwa kusimamia
vizuri fedha kiasi cha shilingi milioni
400 zilizokopwa katika benki ya CRDB mwaka 2008 kwa ajili ya kuendesha shule ya
sekondari Bishop Nkola iliyoanzishwa mwaka 2009 na kusababisha shule hiyo
kupigwa mnada Februari 23,2017 baada ya kushindwa kurejesha deni.
“Baada
ya kuuzwa kwa shule hiyo tuliitisha kikao cha dharura cha baraza la utendaji
tuliunda tume huru kuchunguza jambo hili na baada ya kumaliza uchunguzi wao walileta
taarifa na tumeamua kuchukua maamuzi kwa mujibu wa taarifa hiyo na katiba ya
kanisa letu”,alifafanua askofu Kezakubi.
Alisema
ilibainika kuwa kuuzwa kwa shule hiyo kunatokana na kwamba kulikuwa na matumizi
mabaya ya fedha za mkopo kutoka benki na fedha za harambee mbili zilizofanyika
kanisani hapo na tatizo la kutotoa taarifa kwenye vikao vya ngazi za juu kwani
ngazi za juu zilishtukizwa tu kuwa shule imeuzwa.
“Kwa
sababu ya mzigo wa uongozi na yeye kama msimamizi baraza la utendaji liliamua
kumuomba askofu Nkola astaafu sasa na alipopokea barua hakuwa na maneno ya
kukataa na sisi tunampongeza kuchukua moyo huo kwa kuwajibika”,alieleza askofu
Kezakubi.
Alisema
kosa la askofu Nkola ni kushindwa kusimamia watendaji wake vizuri ili jambo
hilo lisitokee vile alikuwa hajatoa taarifa kwenye mabaraza ya juu kuhusu jambo hilo.
“Askofu
Nkola ameumia kwa sababu ya watendaji wake kutokuwa waaminifu kwani kazi nyingi
zinawaangukia watendaji,askofu hashughuliki na fedha ana majukumu yake,lakini
sasa yanapotokea na kwa sababu yeye ndiyo msimamizi lazima
awajibishwe”,aliongeza askofu Kezakubi.
Aidha
alisema baraza limechukua hatua pia kwa watendaji waliokuwa katika ofisi ya
askofu Nkola ambapo lilimuomba aliyekuwa katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi
ya Shinyanga John Bunangwa ambaye sasa ni askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya
Mwanza naye ajiuzulu nafasi yake ya uaskofu.
Alisema
askofu Bunangwa anachukuliwa hatua kwa kutosimamia vizuri fedha za kanisa
shilingi milioni 400 za mkopo kutoka benki ya CRDB na za harambee iliyoendeshwa
kanisani hapo na waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye.
Askofu
huyo aliongeza kuwa Bunangwa pia alishindwa kusimamia urejeshaji wa mkopo huo
kwa sababu hata akiwepo kulikuwa na matatizo na kushindwa kutumia wataalam
katika kuvunja baadhi ya mikataba alikuwa mwenye anaisimia na kusababisha
hasara kubwa katika kanisa.
Aidha
Bunangwa aliruhusu ongezeko kwenye mikataba mbalimbali bila kufuata utaratibu
wa kuongeza gharama za miradi hiyo.
Katika
hatua nyingine baraza lilimvua uchungaji katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi
ya Shinyanga Jakobo Mapambano kwa kushindwa kupeleka taarifa sahihi katika
vikao vya juu tangu kuanza kwa tatizo la shule.
“Mchungaji
Mapambano pia alishindwa kusimamia vizuri mapato ya shule na fedha za harambee
nyingine iliyofanyika kanisani na kushindwa kukabidhi nyaraka alizoombwa na
tume iliyoundwa na baraza la utendaji kwa ajili ya uchunguzi,na kuweka rehani
magari magari mawili ya kanisa bila kuomba kibali cha baraza la
udhamini”,aliongeza askofu huyo.
Alisema
pia baraza hilo lilimuondoa uchungaji Emmanuel Isaya ambaye alikuwa kwenye
kitengo cha elimu ambapo aliidhinisha malipo kinyume na mamlaka yake na
kushindwa kusimamia ujenzi wa majengo ya shule ambayo yako hali ya chini na
hajakamilika.
Hali
kadhalika baraza hilo lilimwondolea uchungaji Dkt Meshack Kulwa kwa makosa ya
kimaadili na kushindwa kusimamia vizuri ujenzi wa uzio wa shule ambao una ubora
wa chini.
Alisema
tume inaendelea kufanya kazi na yeyote atakayeguswa lazima achukuliwe hatua za
kinidhamu.
“Jambo
hili limeleta aibu katika kanisa letu,kama mtu akiharibu hekalu la mungu naye
mungu atamharibu mtu huyo kwani hekalu la mungu ni takatifu,kanisa ni hekalu la
mungu na yeyote aliyechukua mali ya kanisa arudishe kabla ya kuharibikiwa na
mungu,naomba tuendelee kuliombea kanisa”,alieleza askofu Kezakubi.
Akizungumza
na Malunde1 blog askofu mstaafy wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga Dkt.
John Kanoni Nkola alisema amewajibishwa kutokana makosa yaliyofanywa na
watendaji wake wa chini kwani hata tume iliyoundwa kuchunguza haikuona kama
amehusisha na ubadhirifu wa fedha.
“Kanisa
lina kanuni,sheria na taratibu zake kama kiongozi niliyekuwa naongoza kanisa
nimepokea maamuzi yaliyochukuliwa kwa moyo mweupe kabisa,nimeona kulikuwa na
madhaifu ya kiuongozi,nilitakiwa kustaafu tarehe 25 Mei 2017,nimestaafu kabla
nitaendelea kulitumikia kwa lolote watakalohitaji niwatumikie kama
mstaafu”,alisema askofu Nkola.
Nao
wachungaji waliovuliwa nafasi hiyo walisema wanakubaliana na hatua
iliyochukuliwa kwa kanisa lina sheria,taratibu na kanuni zake.
Aliyekuwa
katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga mchungaji Jakobo Mapambano
alikiri kutenda makosa yaliyotajwa na kuongeza kuwa matatizo katika shule hiyo
aliyarithi mwaka 2010 kutoka kwa aliyekuwa katibu wa kanisa hilo Bunangwa
ambaye sasa ni askofu wa kanisa hilo dayosisi ya Mwanza aliyeombwa kujiuzulu
nafasi hiyo.
Aidha
Mapambano alisema matatizo katika kanisa hilo yanachangiwa na kukosekana kwa
ushirikiano baina ya viongozi na waumini wa kanisa hilo.
Source -Malunde1 blog
No comments