WATANZANIA KUFANYA MIAMALA YA KIFEDHA KUPITIA HALOPESA NA NMB
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Bw. Le Van Dai akisaini mikataba
wakati wa tukio hilo. Kulia niKaimu Mkuu wa Huduma Binafsi za Kibenki wa NMB,
Boma Raballa akisaini tukio hilo
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Bw. Le Van Dai akizungumza katika
tukio hilo la huduma ya Halopesa juu ya kuunganishwa na benki ya
NMB. Kushoto ni Henry Mavulla Mwendesha Biashara wa Halopesa na
kulia ni Kaimu Mkuu wa Huduma Binafsi za Kibenki wa NMB, Boma Raballa.

Kaimu Mkuu wa Huduma Binafsi za Kibenki wa NMB, Boma Raballa akizungumza
juu ya tukio hilo. kushoto ni Henry Mavulla Mwendesha Biashara wa Halopesa
na katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Bw. Le Van Dai.
Kaimu Mkuu wa Huduma Binafsi za Kibenki wa NMB, Boma Raballa akibadilishana nyaraka wakati wa tukio hilo na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Bw. Le Van Dai
Na Frank wandiba
Katika kuakikisha
wanapanua wingo wa huduma za kifedha kwa wananchi wenye kipato cha chini Kampuni
ya mawasiliano ya Halotel kwa kushirikiana na benki ya Nmb wamezindua
huduma ya kufanya mihamala ya kifedha kupitia halopesa hili kuwawezesha
watanzania kunufaika na huduma za kifedha nchi nzima
Akizunguumza katika
halfa ya uzinduzi huo mapema leo jijini dar es salaam Naibu Mkurugenzi wa
kampuni ya Halotel Bwana Le Van Dai alisema ushirikiano huu wa kipekee ambao
umelenga katika kurahisisha maisha ya watanzania hasa waishio vijijini anbao wamekuwa
wakipata tabu kupata huduma za kifedha kutokana na maeneo wanayoishi.
“Tuanatambua
changamoto ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa kikwazo kwa wananchi wengi hasa wa
kipato cha chini kutokana na wengi wao kukwama kuweza kupata huduma za kifedha
kutokana na miundombinu kutowafikia katika maeneo yao” alisema bw Dai.
Pia bwana Dai
aliongeza kuwa azma ya serikali ni kuzitaka taasisi zote
zinazojihusisha na fedha kuwafikia wananchi wote hasa wa maeneo ya vijijini na
kusema kuwa huduma hiyo itapunguza kadhia kwa watumishi wa umma na sekta
nyinginezo anbako huduma za kibenk azijafika.
Alisema kupitia
mawakala wake zaidi ya elfu 30 nchi nzima
huduma hii itawasaidia kuwawezesha wakazi hususani wanaoishi katika maeneo
ambayo hayakuwahikuwa na mawasiliano au huduma za kibenkisasa kuweza kuweza
kupata huduma za kifedha kuotia simu za mkononi.
Kwa upande wake
Kaimu wa huduma Binafsi za kibenki wa NMB bw Boma Rabala alisema ushirikiano
huu ni moja ya mafanikio mengne makubwa ya kibishara kwao hususani katika
kupanua wingo wa utoaji wa huduma zake sambamba na kuwawezesha watanzania wengi
zaidi kupata huduma za kifedha popote walipo.
Alisema kupitia
ushirikiano na kampuni ya mawasiliano ya halotel wana amini wataweza kufikia lengo la serikali
na benki hiyo kuweza kuwafikia wateja wengi zaidi.
Bw Rabala aliongeza ushirikiano huo utasaidia kwa
kiasi kikubwa kurahisisha na kuboresha hali ya maisha na uchumi wa watanzania.
No comments