FARU FAUSTA AZUA BALAA. WABUNGE WAPINGA VIKALI GHARAMA ZA MATUNZO YAKE

Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, wameibuka na kupinga vikali gharama za matumizi ya Faru
Fausta aliyepo katika Hifadhi ya Ngorongoro, na kuongeza kuwa gharama hizo
haziendani na uhalisia.
Mjadala huo uliibuka mara baada ya Mbunge wa
Babati Mjini, Pauline Gekul (Chadema) kuuliza swali kwa Waziri wa Maliasili na
Utalii, Prof. Jumanne Maghembe kuhusu mipango ya Serikali kwa Faru huyo.
Aidha, akijibu swali hilo, Prof. Maghembe
amesema kuwa Faru huyo anatumia gharama kubwa za matunzo kwa sababu ni mzee na
huwa anaugua mara kwa mara.
“Hivi
sasa utafiti unafanyika kwa kumtumia Faru Fausta juu ya namna ya kuishi na
wanyama wa aina hiyo ili waweze kuishi maisha marefu, ni kweli kufanya hivi ni
gharama kubwa sana,”amesema
Prof. Maghembe.
Gharama za matunzo ya Faru Fausta kwa mwezi ni
shilingi milioni 64, kiasi ambacho kiliwashtua baadhi ya wabunge na kutaka
muongozo zaidi wa kupata taarifa za kina zaidi.
Hata hivyo, kwa upande wake Mkuu wa Hifadhi ya
Ngorongoro, Dkt. Fredy Manongi amesema kuwa Faru Fausta ni Mzee na ana umri wa
miaka 54, hivyo alipokuwa porini alikuwa akishambuliwa na Fisi kitendo ambacho
kilimsababishia vidonda vingi.
No comments