DR SLAA AJITATHIMNI KURUD NCHINI. ASEMA UPINZANI USIPOJIPANGA UNAWEZA KUFUTIKA 2020
Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye kwa sasa
anaishi nje ya nchi, Willbrod Slaa amesema anajitathmini kwa kile kilichomfanya
aondoke hapa nchini na familia yake kama hakipo aweze kurejea nyumbani.
Dkt.
Slaa aliamua kuweka pembeni masuala ya siasa baada ya kutofautiana na chama
chake juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa mgombea wa Urais wa Umoja wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.
Amesema
kuwa kwa sasa amemaliza masomo yake na baada ya kutafakari na kujitathmini
atarejea nyumbani muda wowote.
“Ni
kweli nimemaliza masomo yangu, bado napima mazingira yaliyonifanya niondoke na
familia yangu, baada ya hapo nitaangalia uwezekano wa kurejea nyumbani,”amesema
Dkt. Slaa.
Aidha,
kuhusu mwenendo mzima wa Serikali ya awamu ya Tano, amesema kuwa hakuna nchi
hata moja ulimwenguni ambayo Rais wake atakubarika kwa asilimia mia moja, hivyo
Rais Magufuli ameonyesha msimamo wa kusimamia kile anachokiamini
Hata
hivyo, ameongeza kuwa kama wapinzani hawatakuja na ajenda makini na mkakati
unaoweza kuwasaidia wananchi hapo walipo, basi upinzani unaweza kufutika mwaka
2020.
“Kama
nilivyorejea mara kadhaa, upinzani makini utaingia Ikulu kwa ajenda mbadala.
Ajenda makini yenye kuwalenga wananchi moja kwa moja katika kuwatoa kwenye kero
zao mbalimbali.
“Hadi
sasa ninachoona ni ‘kurukia’ kauli za JPM, lakini kauli si ajenda na hatupeani
maksi kwa kuzungumzia usahihi wa lugha. Wako wanaotazama usahihi wa lugha na
mahali pa kutazama usahihi huo. Kimsingi hayo ni masuala ya darasani au kwenye
uandishi wa vitabu.
“Aidha
kumtuhumu JPM kukiuka Katiba na sheria nayo haina tija. Wote wanaomtuhumu
wanajua kuwa wakiambiwa waonyeshe kifungu mahususi alichokiuka yeye mwenyewe
katika utendaji wake hawana majibu ya kuridhisha.
“Hivyo
mimi sijaona mwenendo wa JPM unaosaidia kuingiza upinzani Ikulu. Isitoshe kama
hawatakuja na ajenda makini na mkakati ulioandaliwa unaowatoa wananchi hapa
walipo kwenda kwenye raha, upinzani unaweza kufutika kabla ya 2020,”alisema Dk.
Slaa.
No comments