JAJI MKUU AMPA MAJUKUMU TUNDU LISSU
Kaimu Jaji Mkuu wa
Tanzania, Profesa Ibrahim Juma ameutaka
uongozi mpya wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kuusoma na kuuelewa mpango
mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania ili umoja huo uweze kuchangia
katika kuutekeleza.
Aliyasema hayo jana
alipotembelewa na uongozi wa TLS
ulioongozwa na Rais wa chama hicho,
Tundu Lissu.
Alisema ni vema kuusoma Mpango Mkakati huo kufahamu ni wapi mahakama inatoka na wapi
inapotaka kuelekea hususan katika suala
zima la maboresho ya huduma ya utoaji haki nchini.
Mpango Mkakati wa
Mahakama ya Tanzania (2015/2016-2019/2010) umegawanyika katika nguzo kuu tatu
ambazo ni utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali.
Nyingine ni
upatikanaji na utoaji haki kwa wakati na kurejesha imani ya jamii na
ushirikishwaji wa wadau na umejikita katika kuboresha huduma za utoaji haki kwa
ujumla.
Naye Rais wa TLS,
Tundu Lissu pamoja na mambo mengine
alieleza baadhi ya changamoto zinazowakabili mawakili nchini .
Alisema changamoto
hizo ni pamoja na baadhi ya mahakama
kutokuwa na ofisi kwa ajili ya mawakili, taratibu za usajili wa mawakili, na
nyingine.
Akijibu, Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Ilvin Mugeta alisema Mahakama Kuu inaendelea kufanyia kazi
changamoto zote zinazowakabili mawakili.
Mugeta alisema
kingine kinachoangaliwa ni kuona
uwezekano wa taratibu za malipo kufanyika kwa elektroniki.
No comments