WAZIRI DK.CHARLES TIZEBA KUFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA KILIMO JIJINI DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Kilimo
,Chakula,Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba (pichani), anatarajia kufungua
kongamano la siku tatu la wadau wa sera
za kilimo kesho jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kampuni ya Agricultural Non State Actors
Forum (ANSAF), Audax Rukonge, alisema serikali imekusudia kuweka kipaumbele
kwenye viwanda vya uchakataji wa mazao ya kilimo.
Kongamano hilo
litahudhuriwa na wadau zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali pia litalenga
kuongeza uelewa miongoni mwa watunga sera kuhusu mchango wa kilimo katika
kuhamasisha ukuaji wa viwanda Tanzani.
“Wadau watajadili kupata tafsiri halisi ya sekta ya
uchakataji mazao ya kilimo katika muktadha wa mageuzi ya viwanda Tanzania,”alisema
Rukonge alisema
kongamano hilo limedhaminiwa na USAID, Benki ya Dunia, ANSAF, JICA na wadau
wengine ambao wamesaidia kuleta watalamu wakiwamo wakulima,
watafiti,wafanyabiashara na watunga sera.
Mratibu wa Jukwaa la
Sera ya Kilimo na Mchumi mwandamizi Wizara ya Kilimo, Sophia Mlote alisema
kongamano hilo la tatu litajadili maendeleo ya kilimo nchini ikiwamo kujadili
namna ya kutetea sera, sheria, kanuni.
Pia alisema kongamano
hilo litajikita katika kujadili juu ya mpango wa kilimo cha mihogo, mikunde,
samaki, mazao, usafirishaji pamoja na vifungashio kwa kuwa wazalishaji wengi
hawana vifungashio.
No comments