TAASISI YA ECONOMIC DIPLOMACY (TRAINING ACADEMY) YAWANOA MAAFISA KUTOKA SERIKALINI, VYUO VIKUU NA SEKTA BINAFSI
Taasisi
isiyo ya kiserikali ya ECONOMIC DIPLOMACY – TRAINING ACADEMY imeendesha mafunzo
ya siku saba ya Itifaki na Uhusiano ya Kibiashara ‘PROTOCOL AND BUSINESS ETIQUETTE SHORTCOURSE
kwa ajili ya kuwajengea uwezo maafisa kutoka serekalini na sekta binafsi.
Akiongea
wakati akifunga mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa ECONOMIC
DIPLOMACY –TRAINING ACADEMY Ndugu Lucas Jackson alisema Mafunzo hayo ni
muendelezo wa mafunzo ya muda mfupi
yatolewayo na ECONOMIC DIPLOMACY –TRAINING ACADEMY kila mwezi kwa maaaafisa kutoka taasisi
mbalimbali kwa lengo la kuwajegea uwezo,
Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa ECONOMIC DIPLOMACY –TRAINING ACADEMY Ndugu Lucas
Alisema
mafunzo hayo ya muda mfupi ambayo Kwa kawaida wawezeshaji wake huwa ni mabalozi na wakufunzi waliobobea
katika mambo ya Diplomasia na hivyo kuwapa washiriki uzoefu na mafunzo ya
kiutendaji zaidi ili kuwajengea uwezo na ufanisi katika kuboresha majukumu yao.
Bw
Jackson aliongeza kuwa washiriki watafundishwa jinsi ya kuratibu itifaki za
dhifa, sherehe za kitaifa na mikutano mingine mbali mbali pamoja na kuandaa
mikutano ya kibiashara, tabia njema za kibiashara, kanuni za Mavazi na kupokea
wageni mashuhuri na kuwahudumia.
Alisema
washiriki watajifunza kuhusu Diplomasia,
uhuisiano wa umma na namna bora ya kuandaa taarifa kwa ajili ya mawasiliano na
umma, yalihusisha maofisa 24 wa kada mbalimbali kutoka idara za Serikali , vyuo
vikuu na sekta binafsi pamoja na maafisa kutoka katika Balozi zinazowakilisha
nchi zao Tazania.
Picha baadhi ya
washiriki kutoka The Open University of Tanzania wakiongozwa na Dr. Celia
Muyinga –wa kwanza kulia- wakiwa na vyeti vyao
Aidha
bw Jackson alisema mafunzo hayo yatawasaidia maofisa hao kuboresha utendaji wao
wa kazi na kuleta ufanisi mahala pa kazi hivyo kutoa rai kwa waajiri kuwaruhusu
wafanyakazi wao kushiriki mafunzo hayo yanatolewayo na taasisi EONOMIC
DIPLOMACY –TRAINING ACADEMY ili kuwajengea uwezo hasa katika Diplomasia ya
Uchumi na uchumi wa viwanda Tanzania, na hivyo kuzalisha wataalam wenye weredi
wa uchumi wa viwanda na Diplomasia ya Uchumi.
Alisema
tasisi yake imepanga tena kuendesha Mafunzo mengine ya wiki moja jijini dar es
salaam ya UTATUZI WA MIGOGORO NA USULUHISHI (CONFLICT RESOLUTION) tarehe 22 -25
mwezi huu, yatakayofuatiwa na DIPLOMASIA YA UCHUMI, Biashara na uwekezaji
(ECONOMIC DIPLOMACY: Trade and Investment Promotion) tarehe 5 – 8 April, 2017.
Ametetoa
wito kwa wale wote ambao wangependa kushiriki mafunzo hayo kuwasiliana na
taasisi hiyo kupitia namba 0713667303 au lucassoona@yahoo.com kwa maelezo zaidi
na kupewa utaratibu
No comments