Breaking News

TRUMP AMTUMBUA KAIMU MWANASHERIA MKUU BAADA YA KUPINGA AGIZO LAKE



Rais wa Marekani, Donald Trump amemfuta kazi Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Sally Yates saa chache baada ya  kiongozi huyo kuwaagiza Mawakili kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo vya kuingia Marekani raia wa nchi saba zenye waislamu wengi.

Sally Yates aliyeteuliwa na Rais Obama alisema kuwa alitoa agizo hilo kwa Mawakili sababu haamini kama zuio la raia kuingia Marekani ni halali.

Rais Trump Ijumaa alitia saini amri inayozuia raia kutoka Somali, Sudan, Libya, Yemen, Iran, Syria na Iraq kuingia nchini Marekani ambapo zuio hilo ni la siku 90.

Maandamano yamezuka maneneo mbalimbali ya Marekani huku wakipinga zuio hilo. Wanadiplomasia wamesema kuwa zuio hilo huenda likasababisha hatari zaidi kwa usalama wa Marekani.

 Aidha, baadhi wamehoji kwanini zuio limewekwa kwa nchi hizo saba wakati kwa miaka ya hivi karibuni hakuna raia wake aliyehusika na ugaidi nchini Marekani?

Rais Trump amevikosoa vyombo vya habari vinavyopotosha kuwa  zuio hilo ni kwa Waislamu pekee. Rais Trump amesisitiza kuwa zuio hilo ni kwa raia wote wanaotoka katika nchi hizo hata kama si Waislamu.

Trump alisaini amri hiyo katika kile alichosema kuwa ni kuzuia watu wenye misimamo mikali kuingia nchini Marekani ikiwa ni hatua za kuimarisha ulinzi na usalama.


No comments