CUF YATOLEA UFAFANUZI SAKATA LA RUZUKU YA CHAMA HICHO
Chama cha wananchi CUF bara kimetoa ufafanuzi juu ya
sakata la ruzuku ya chama hicho ambayo ilipokelewa kupitia akaunti ya Nmb bank
tawi la Temeke jijini Dar es salaam.
Akizumgumzia sakata hilo mkurugenzi wa fedha na uchumi
Taifa wa chama hicho Bw.Thomas Malima alisema ofisi ya msajili wa
vyama vya siasa nchini imewapa ruzuku hiyo kwa mujibu wa sheria ya vyama ya
mwaka 1992 na kusema kuwa ruzuku hiyo ilikuwa imezuiliwa kwa muda wa miezi
minne kuanzia mwezi Septemba hadi Desemba 2016 kutokana na sintofahamu
ya uongozi wa kitaifa CUF
Alisema takribani mwaka mmoja sasa tangu mwenyekiti Taifa wa
chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba kuwa nje ya uenyekiti ambapo ruzuku zote
zilisitishwa kwa upande wa wilaya za Tanzania bara wakati Zanzibar ikiendelea
kupokea ruzuku hiyo na kudai kuwa jambo hilo ni uonevu kwa wanacuf wa Bara na kueleza
kuwa mpango huo ulikuwa wa makusudi wa maalim Seif na genge lake.
Bw. Malima alisema jumla ya shilingi 66,300,000 ya fedha
ya ruzuku hiyo mara baada ya kelewa zilipelekwa katika wilaya 82 za Tanzania
bara kati ya wilaya 104 ambazo zina viongozi halali wa chama.
Pia bw Malima alisema wilaya zilizobaki 22 bado
hazijapatiwa mgao wa fedha hizo kutokana na akaunti zao kuwa na matatizo
mbalimbali na kutoa wito kwa viongozi wa chama cuf katika wilaya hizo kuhakikisha
akaunti hizo zinakuwa sawa ili waweze kupatiwa fedha.
Katika hatua nyingine Bw Malima amewataka viongozi wa Cuf
kuzingatia matumizi sahihi ya fedha hizo kwa mujibu wa katiba ya chama hicho na
sheria ya nchi kwakuwa hizo ni fedha za umma.
Bw Malima ameelezea kusikitishwa na tamko la Inayojiita
bodi ya wadhamini wa Cuf kudai kuwa fedha hizo zimeibwa na kuwataka viongozi wa
wilaya zote nchi kutokupokea fedha hizo, kwa mujibu wa ibara ya 98(1) inafafanua
kuwa bodi hiyo iliteuliwa 2010 na kumaliza muda wake 2015 na baada ya hapo
haikuwahi kuteuliwa tena wala kulipiwa mchango wa kila mwaka Rita tangu mwaka
2013
No comments