TANZANIA KUADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA AFRIKA MACHI 3.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustine Kamuzora akizungumza na waandishi
wa Habari juu ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Afrika itakayofanyika tarehe
3 Machi, 2017.Kulia kwake ni Mkurugenzi
wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.Richard Muyungi.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof.Faustine Kamuzora akifafanua jambo wakati wa
mkutano na waandishi juu ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Afrika
itakayofanyika tarehe 3 Machi, 2017. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira
Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.Richard Muyungi. Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.
Na
Daudi Manongi-MAELEZO
Tanzania
inategemea kuadhimisha siku ya Mazingira Afrika, Machi 3, 2017 ambapo siku hiyo
imetengwa kukumbuka umuhimu wa kutunza na kuhifadhi mazingira Barani Afrika.
Hayo
yamebainishwa na katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof.Faustine Kamuzora
wakati akiongea na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam juu ya
maadhimisho hayo ambapo kitaifa yanategemewa kufanyika wiki ya kwanza ya mwezi
wa sita.
Ameongeza
kuwa Azimio la kuadhimisha Siku hiyo lilipitishwa na kuamuliwa na Baraza la
Mawaziri wa Mazingira wa nchi za Afrika (AMCEN) kwenye mkutano uliofanyika
Durban, Afrika Kusini mwaka 2002.
“Siku
hii iliamuliwa iwe kielelezo cha kukuza weledi kuhusu kupambana na uharibifu wa
mazingira pamoja na kuenea kwa hali ya jangwa katika bara letu. Aidha siku hii
ilikuwa inaadhimishwa nchini Ethiopia kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika,”
alisema Prof. Kamuzora.
Aidha
Prof.Kamuzora amewataka watanzania kushiriki katika maadhimisho hayo katika
kukabiliana na uhalibifu wa mazingira unaosabishwa na matumizi yasiyoendelevu
ya bioanuai na rasilimali zake.
“Kila
mtu afanya shughuli za kiuchumi zisizoharibu mazingira ikiwa ni pamoja na
kutumia nyenzo za uvuvi endelevu, kutumia nishati jadilifu, majiko sanifu na
banifu, nishati mbadala, kudhibiti uchafu wa mazingira, kupunguza uzalishaji wa
taka na kusimamia ukusanyaji wa taka ili kuhakikisha miji yetu inakuwa safi,”
alifafanua Prof. Kamuzora.
Aidha
amewakumbusha viongozi kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa kutumia fursa hiyo
kuzihuisha kamati za Mazingira ili ziweze kusimamia shughuli za utunzaji
mazingira katika maeneo yao ya Mikoa, Halmashauri za Wilaya, Sekta zote pamoja
na Taasisi mbalimbali, mashirika yasiyo ya Kiserikali na Wananchi wote kwa
ujumla kuhakikisha wanahamasishwa kushiriki katika shughuli za hifadhi na usafi
wa Mazingira.
No comments