MBUNGE PAULINA GEKUL ANUSURIKA KIFO AMELAZWA ICU, ZIARA YAAHIRISHWA
Mbunge
wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul amenusurika kifo baada ya gari lake
lenye namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka vibaya ambapo mbunge
huyo alikuwa katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira Luhaga Mpina wilayani
Babati mkoa wa Manyara.
Baada
ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye ni mmbunge wa babati mjini
akakimbizwa hospitali ya mkoa wa manyara na kulazwa katika chumba cha wagonjwa
mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa kuingia katika chumba hiki na
madakatari ambao wanamuhudumia mbunge huyo
Hata
hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa mazingira amelazimika kuahirisha
ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa babati huku mpina
akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati kwa kutambua umuhimu wa kutunza
mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari kwaajili ya kubebea taka
lenye thamani ya zaidi ya milioni 200.
No comments