SAKATA LA UAMSHO LAIBUKA TENA, MBUNGE ATAKA KUJUA SABABU ZA KUENDELEA KUSHIKILIWA ILHALI USHAHIDI ULISHAKOSEKANA
Sakata
la masheikh wa Uamusho walioshtakiwa kwa tuhuma za ugaidi, limeibuka bungeni
jana baada ya Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF) kuhoji ni nchi gani
ambayo haina tishio la kigaidi inaweza kuwa na mlundukano wa watu wenye makosa
hayo kwenye magereza.
“Hapa
katika jibu nimeambiwa siku 60 zinatosha kutoa ushahidi na kwamba, kama
ushahidi haukupatikana, watuhumiwa waachiwe. Lakini masheikh wa Uamsho wana
miaka minne sasa wapo katika magereza na ushahidi umeshindwa kupatikana,”
alisema Khatib.
Alihoji
iwapo watuhumiwa hao wanawekwa mahabusu kwa
kuwa
wana kesi ya kujibu, au kwa amri ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
(SMZ).
“Waziri
wa vikosi vya SMZ Zanzibar na Makamu wa Rais Zanzibar wamewahi kunukuliwa
wakisema kwamba waliwaleta masheikh Tanzania ili wanyee ndoo katika magereza ya
Tanzania Bara.” Alisema Khatib Said Haji
Akijibu
swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yusuph Masauni alisema kesi
za watuhumiwa hao zipo mahakamani na kwa taratibu hawaruhusiwi kujibu hoja
kortini.
Hali
hiyo ilisababisha baadhi ya wabunge kuguna bungeni hali iliyomfanya Waziri wa
Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe kuongezea majibu ya swali hilo.
Dk
Mwakyembe alisema ni kweli kwamba sheria inataka mahakama kama upelelezi
haujakamilika ndani ya siku 60, mtuhumiwa kuachiwa huru, lakini Mkuu wa
Upelelezi wa Mkoa (RCO) anaweza kupeleka maombi mahakamani ya kuongezwa siku.
Alisema
baada ya hapo suala linakuwa chini ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na kwamba,
kulingana na uzito wa shtaka anaweza kuomba kuongeza muda.
“Suala
la ugaidi si dogo ni la kimtandao na kuutambua huo mtandao si suala dogo,”
alisema Dk Mwakyembe
No comments