VIPINDI MAALUM VYA RADIO KUPINGA UKATILI VYA ZINDULIWA
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga akikata
utepe kuashiria mwanzo wa urushaji vipindi maalumu vya
kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga akijiweka tayari kurusha kipindi maalumu cha kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga akijiweka tayari kurusha kipindi maalumu cha kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga akiiongea na
wananchi ndani ya gari la matangazo la RADIO TIMES mara baada ya kuzindua
vipindi maalumu vya kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Na Frank Wandiba
Wizara
ya Afya, Idara kuu Maendeleo ya Jamii leo imezindua wa vipindi maalumu vya
Radio ambavyo vinalenga kuelimisha jamii kuacha vitendo vya ukatili dhidi ya
wanawake na watoto hapa nchini.
Vipindi
hivi vitakuwa vikirushwa na Radio maalufu nchini ‘RADIO TIMES 100.5 FM ambayo
itashirikiana na wataalamu wa Wizara kusimamia na kuratibu maandalizi ya
uendeshaji wa vipindi vya elimu na stadi za kuzuia ukatili wa kijinsia katika
jamii.
Akaiongea
katika sherehe fupi ya uzinduzi wa vipindi hivyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Idara kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga amesema ubunifu wa vipindi hivi
na Radio Times 100.5 ni sehemu ya
mwitikio wa tasnia ya habari katika kutekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa
Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto ambao ulizinduliwa Desemba,
2016.
Ameongeza
kuwa uzinduzi wa vipindi maalum vya elimu kwa umma ni kielelezo thabiti kwamba
RADIO TIMES FM inadhamira ya dhati ya kusaidia juhudi za Serikali kuimarisha
ulinzi na usalama wa mama na mtoto.
Bi
Sihaba aliendelea kusema kuwa anatambua
kuwa REDIO TIMES FM ni chombo binafsi ambacho kimetambua kuwa kinaowajibu wa
kuhakikisha kuwa wanawake na watoto katika nchi yetu wanafurahia upatikanaji wa
haki zao na wanaishi katika mazingira salama.
Pia
amewapongeza wanahabari wa vyombo vyote vinavyoelimisha na kuhamasisha jamii
kuhusu athari za ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kujadili afua
zinazotakiwa kuchukuliwa katika kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto na
madhara ya ukatili huo.
Aidha
ametoa rai kwa vyombo vingine vya habari kufuata nyayo za Radio Times FM katika
kukuza uelewa wa jamii kuhusu athari za ukatili dhidi ya wanawake na
watoto.
Katibu
Mkuu huyo ametaja ukatili kuwa na athari
ambazo huwapunguzia uwezo wanawake na watoto katika kupata haki ya
kushiriki shughuli za uzalishaji kwa uhuru na amani huku akaizitaja takwimu za
Jeshi la Polisi kuwa zinaonesha vitendo vya ubakaji kwa mwaka 2015 vilifikia
3,444 na matukio ya shambulio, kujeruhi na matusi vilikuwa14,561.
Aidha
utafiti wa Idadi ya Watu na Afya ya mwaka 2010 inaonesha kuwa asilimia 39 ya
wanawake wa umri wa miaka 15 – 49 walifanyiwa ukatili wa shambulio na vilevile
Taarifa ya Utafiti wa Ukatili dhidi ya Watoto ya mwaka 2011 ilibainisha kuwa
asilimia 72 ya wasichana na asilimia 71 ya wavulana nchini walifanyiwa ukatili
wa vipigo.
Taarifa
hiyo pia imebainisha kuwa mtoto 1 kati ya watoto 3 wa kike na mtoto 1 kati ya
watoto 7 wa kiume walifanyiwa ukatili wa kingono. Aidha, takwimu zinaonesha kuwa watoto 15 kati
ya watoto 100 wa kike hapa nchini wamefanyiwa ukeketaji.
Kwa
ujumla takwimu hizi zinaonesha jinsi gani tatizo hili lilivyokubwa katika jamii
zetu, hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kuchukua hatua thabiti kuzuia ukatili
huo aliendelea kusema.
No comments