MHE MAKONDA AMTAJA VIGOGO WENGINE NA WASANII WAWILI MSALA DAWA ZA KULEVYA, ATOA AGIZO KWA WALIOKAIDI KURIPOTI LEO WAKAMATWE
Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam ameagiza kukamatwa kwa watu aliowataja jana kuhusika
na dawa za kulevya ambao hawajajisalimisha kituo cha polisi leo, kama
alivyoagiza
Makonda
aliyefika katika Kituo Kikuu cha Polisi, amesema watu wao ambao
hawajajisalimisha, wasakwe kokote waliko, na wawekwe ndani.
"Kuna
watu tuliwaita, baadhi nimeambiwa hawajafika, ambao hawajafika nimeagiza
wakachukuliwe wakae ndani mpaka siku ya Jumatatu" Amesema Makonda.
Amesema
kati ya watu waliotajwa jana, ni wasanii watano pekee ndiyo wamejisalimisha
siku ya leo katika kituo hicho wakiongozwa na aliyewahi kuwa Miss Tanzania Wema
Sepetu, Nyandu Tozi (Hamidu), TID, Babuu wa Kitaa.
Pia
kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo, jumla ya polisi 7 wamekwisha kamatwa huku
watatu wakiendelea kutafutwa na wengine wawili ambao hawako katika jiji la Dar
es Salaam watakamatwa ndani ya muda mfupi ujao.
Katika hatua nyingine, Makonda ametaja orodha
nyingine tofauti na aliyoitaja jana ya watu wanadaiwa kuhusika katika dawa za
kulevya akiwemo msanii bongo fleva Vanessa Mdee, mwanamitindo anayefahamika kwa
jina la Tunda.
Mbali
na wasanii hao, makonda amewataja pia askari wengine watatu wa Jeshi la Polisi
Tanzania ambapo amedai kuwa askari hao wanatuhumiwa kwa kupokea pesa kiasi cha
shilingi bilioni 1 hivi karibuni kutokana na kuhusika na dawa za kulevya pamoja
na kukamata dawa za kulevya kisha kuziuza tena.
Pia
amemtaja anayejulikana kwa jina la Omari Sanga kuwa ni mmoja anayehusishwa na
uletaji wa dawa ya kulevya na amesababisha asilimia 60 ya watanzania kufungwa
katika magereza ya china.
Makonda
amesema "Waliofika tutajadiliana nao kuona namna gani wanatupatia yale
tunayoyataka kuyafanyia kazi kutokana na taarifa tulizo nazo. Vita hii ya dawa
za kulevya haiishi leo, inaisha pale dawa zinapokuwa zimeisha"
Naye
Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kamishna Simon Sirro amesema kuwa Jeshi
hilo limeunda tume ya kushughulika na mapambano dhidi ya dawa za kulevya mkoani
humo
No comments