KAMANDA SIRO AMJIBU MBOWE, ASEMA KAMA HATARIPOTI POLISI, ATAMFUATA POPOTE ALIPO
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kama Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hataripoti bila kutoa taarifa yoyote ya udhuru atafuatwa kwa kuwa jeshi hilo linahitaji kumhoji.
Kamanda
wa kanda hiyo, Simon Sirro amesema hayo leo muda mfupi baada ya Mbowe kueleza
kuwa hataripoti polisi kutokana na wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda.
Amesema
operesheni dhidi ya mihadarati bado inaendelea na kuanzia sasa hawataruhusu
tena mkusanyiko wa watu katika kituo cha polisi kati na wale watakaoonekana
watashughulikiwa hivyo asije kulalamika mtu kwani taarifa imeshatolewa.
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza rasmi kutofika kituoni hapo kwa madai kuwa
hawezi kwenda polisi kwa wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda isipokuwa pale tu
taratibu za kisheria zitakapofuatwa.
No comments