IRAN KUADHIMISHA WIKI YA UTAMADUNI KWA MAONYESHO JIJINI DAR.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bibi. Zamaradi Kawawa akizungumza
wakati wa Mkutano baina ya waandishi wa habari, wawakilishi kutoka Kituo cha
Utamduni cha Irani pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo
jijini Dar es Salaam.Kituo cha utamaduni cha Iran kimeaandaa maonyesho ya
utamaduni yatakayofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, kuanzia terehe
10 - 12 Februari kwa kuonyesha tamaduni kutoka Iran.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Hajjat Shani Kitogo (wa pili kutoka kulia)
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonyesho ya Utamaduni wa Iran leo
jijini Dar es Salaam.
Mshauri
wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Iran nchini Ali Bagheni akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya utamaduni wa Iran
inayotarajiwa kufanyika kuanazia tarehe 10 – 12 Februari leo jijini Dar es
Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bibi. Zamaradi Kawawa akiwa katika
picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Kituo cha Utamduni cha Iran walioambatana
na wasanii kutoka Irani pamoja na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
No comments