HUZUNI NA SIMANZI VYATAWALA MAHAKAMANI. WAKATI DAKTARI AKITOA USHAHIDI DHIDI YA SCORPION
Daktari Bingwa wa Macho wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Christine
Mataka ambaye alimpokea na kumhudumia, Said Mrisho anayedaiwa kutobolewa macho
na Salum Njwete maarufu Scorpion akiwa shahidi wanne katika kesi hiyo upande wa
serikali, ametoa siri nzito ya tukio hilo.
Dokta Mataka amesema alikuwa daktari wa kawaida kwa muda mrefu lakini
alitunukiwa digrii ya pili (Master’s) na kuwa daktari bingwa wa matatizo ya
macho miaka 14 iliyopita.
Akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nasoro Katuga bingwa huyo
alisema macho ya Said hayakutobolewa kama inavyosemwa na watu kwenye vyombo vya
habari isipokuwa yamenyofolewa na kuondolewa kabisa.
Majeruhi alifika hospitali macho yake yakiwa yamenyofolewa na kubaki
hukohuko,hospitali hakufika hata na mabaki ya goroli.
Akielezea kitaalamu Dokta Mataka alisema kwa kawaida mtu anapotobolewa
macho na kitu chochote ni lazima ukute goroli zikiwa zimepasuka na utete wenye
utelezi unakuwa umetapakaa machoni lakini kwa majeruhi huyo goroli za macho
yote mawili zilikuwa hazipo kabisa.
"Ukweli
hiyo hali ilinishangaza sana kwa miaka 14 nikiwa kama daktari bingwa wa macho
sijawahi kukutana na tukio kama hilo hivyo baada ya kupigwa na butwaa
niliwapigia mabingwa wenzangu waje kujionea hali hiyo na tushauriane jinsi ya
kufanya.
"Hata
wao walivyofika wote walishangaa na kuniambia nao hawajawahi kukutana na hali
hiyo.
"Nilimtibia
majeruhi wakati huo huo nilikuwa nikimuongelesha na kumuuliza yaliyomsibu
ambapo aliniambia wakati akinunua kuku pale Buguruni ndiyo akatokea mtu na
kuanza kumshambulia.
"Nikamuuliza
kama anamfahamu hiyo mtu aliniambia akimuona atamtambua.
"Baada
ya matibabu nilimpeleka wodini na kumuandikia tarehe za kuhudhuria kliniki na
nilimuambia kuwa katika maisha yake hawezi kuona tena hivyo ajifunze kuishi
maisha ya mtu asiye na macho.
"Baadae
alipoanza kuja kliniki aliniambia kuwa mama yake alikuwa akitaka kumpa jicho
lake moja lakini nilimueleza ukweli kuwa hilo haliwezekani.
"Huwezi kulihamisha
jicho halafu likawa hai hiyo huduma haipo hapa duniani.
Baada ya kutoa ushahidi wake mbele ha Hakimu Frola Haule kesi hiyo
iliahirishwa mpaka Februari 22 mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo
ambapo daktari bingwa wa tumbo ambaye nae alimtibu majeruhi huyo anatarajiwa
kutoa ushahidi wake kwa upande wa serikali.
No comments