Breaking News

UWAKITA UMEIOMBA SERIKALI KUTINGILIA KATI SWALA LA URASIMISHAJI WA NEMBO YA AL-HALAL

Mwenyekiti wa Umoja wa wainjilisti wa madhehebu ya kikristo Tanzania (UWAKITA), bwana Samson Bullegi

Umoja wa wainjilisti wa madhehebu ya kikristo tanzania (UWAKITA) umeiomba serikali kutingilia kati swala la urasimishaji wa nembo ya al-halal itakayotumiwa na waumini wa dini ya kiislam kutambua bidhaa ikiwemo vyakula ambavyo vimeandaliwa kwa kufata misingi ya dini hiyo nchini.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini dar es salaam mwenyekiti wa Umoja  bwana Samson Bullegi alisema kamwe umoja huo haupingi kuwepo kwa nembo hiyo bali unapiga urasimishaji wa nembo hiyo ya al-halal, na jinsi itakavyokuwa unafanya kazi zake hapa nchini.

Alisema umoja huo hauna tatizo na dini nyingne hapa nchini isipokuwa kauli iliyotolewa na bakwata mwishoni mwa mwaka jana kwa waandishi wa habari juu ya hatua yao ya kuwepo na mpango wa kurasimisha nembo hiyo ya al-halal nchini.

Bw Bullegi aliongeza kuwa kwa mujibu wa sheria na katiba ambazo zinatambua mamlaka ya chakula na dawa (TFDA), na Shirika la viwango (TBS) kama wasimamizi wa maswala la uasalama wa chakula na viwango nchini ivyo kitendo cha kurasimisha nembo hiyo ni kukiuka sheria.
Katibu mkuu wa umoja wa wainjilisti wa madhehebu ya kikristo Tanzania (UWAKITA), Bw Cecil Simba Ulenga akifafanua jambo

Kwa upande wake katibu mkuu wa unoja huo Bw Cecil Simba Ulenga alisema rejea ripoti ya umoja huo ambayo imetolewa hivi karibuni kuonyesha kuwepo kwa vishairi a vya uvunjifu wa amani nchini kufatia kuripotiwa matukio hayo katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema hipo haja kwa serikali kuliangalia kwa mapana zaidi swala hilo pamoja kulishughulikia kwa busara zaidi hili kuweza kulimaliza kwa amani na pande zote mbili kupata muafaka wa kudumu kwa manufaa ya taifa.

No comments