Breaking News

BREAKING NEWS: YUSUPH MANJI ATOKA NDANI NA KUCHUKULIWA NA GARI YA WAGONJWA.

 Mfanyabiashara maarufu na Mwenyekiti wa Club ya soka ya Yanga Yusuph Manji ambaye alikua akishikiliwa na Polisi kituo cha kati Dar es salaam toka Alhamisi ya February 9 2017 baada ya kwenda kuhojiwa kutokana na kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe  Paul Makonda kwenye orodha ya watu 65 kwenye sakata la dawa za kulevya.

Manji ambaye alikwenda Polisi toka Alhamisi iliyopita kwa ajili ya kuitika wito wa mkuu wa mkoa baada ya kuwataka kuripoti siku ya ijumaa kwa ajili ya mahojiano kituoni hapo, Leo jioni ameonekana na Waandishi wa habari nje ya kituo cha Polisi kati Dar es salaam akichukuliwa na gari la Wagonjwa lenye namba za usajili za DFP na kuondoka nae.
Mfanyabiashara huyo amechukuliwa na gari la kubebea Wagonjwa na haijajulikana limempeleka wapi lakini alionekana akitembea mwenyewe  na kuingia kwenye gari hilo (Land Cruise Nyeupe) bila kubebwa au kusaidiwa huku gari lake aina ya Range Rover likitangulia mbele na watu wengine.
Katika msafara huo uliondoka kituoni hapo sambamba na gari yake aina ya Range Rover lakini yeye mfanyabiashara huyo alipanda gari la Wagonjwa. 

Source Millard Ayoo

No comments