YANGA YATUPWA NJE KOMBE LA MAPINDUZI NA SIMBA KWA PENATI YA 4-2, FAINALI NI SIMBA VS AZAM
Yanga
imeendelea kusulubiwa kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup baada ya kujikuta
ikichezea kichapo kutoka kwa Simba kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili kwa
mikwaju ya penati 4-2 kufatia dakika 90 kumalizika bila timu hizo kufungana.
Baada
kichapo cha 4-0 kutoka kwa Azam FC, Yanga imeondoshwa kwenye michuano hiyo na
kuziacha Simba na Azam zikutane kwenye mchezo wa fainali ambao utachezwa siku
ya Ijumaa January 13, 2017 ikiwa ni siku moja baada ya kilele cha Mapinduzi ya
Zanzibar.
Golikipa
wa Simba Daniel Agyei ndio alikuwa shujaa kwa upande wa Simba hususan kwenye
changamoto ya mikwaju ya penati. Agyei ameokoa penati mbili za Deogratius
Munishi na Mwinyi Haji huku yeye akifunga penati yake baada ya Mkude kufunga ya
kwanza.
Wachezaji
wa Simba waliofunga penati: Jonas Mkude, Daniel Agyei, Mzamiru Yassin na Javier
Boukungu
Method
Manjale ni mchezaji pekee wa Simba aliyekosa penati ambayo iliokolewa na
golikipa wa Yanga Deogratius Munishi.
Simon
Msuva na Thaban Kamusoko ndio wachezaji pekee wa Yanga waliofunga penati zao
huku Deogratius Minish ‘Dida’ na Mwinyi Haji penati zao zilitua kwenye mikono
ya golikipa wa Simba Daniel Agyei.
|
No comments