RAIS SHEIN KUONGEZA MSHAHARA WA WATUMISHI KWA ASILIMIA 100 VISIWANI ZANZIBAR
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
ametangaza neema mpya kwa wafanyakazi visiwani humo baada ya kuwakikishia
kupandisha kima cha chini cha mshahara kuanzia mwaka huu (2017).
Dkt.
Shein ametoa hakikisho hilo jana wakati akiwaongoza watanzania kuadhimisha
Miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika sherehe zilizofanyika katika
uwanja wa Amani visiwani humo.
Alisema
kuanzia mwaka huu kima cha chini cha mshahara kitaongezeka kutoka Tsh. 150,000
hadi Tsh. 300,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 100.
Dkt.
Shein alitoa tathmini yake ya mwaka mmoja tangu achanguliwe tena kuiongoza
Zanzibar, ambapo alisema mwaka 2016 umekuwa ni wa mafanikio makubwa katika
nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, kilimo, viwanda, huduma za jamii ikiwemo afya
na huduma za maji, miundombinu n.k.
Akihutubia
kwenye uwanja wa Amani Dkt. Shein alisema, serikali yake itaendelea kudumisha
na kuenzi umoja na mshikamano ambao uliasisiwa na viongozi wa mapinduzi hayo.
Alisema,
mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kukuza pato la taifa hadi kufikia 6.6%
licha ya kuongezeka kwa mfumuko wa bei kutoka 5.7% katika mwaka 2015 hadi
kufikia 6.7% mwaka 2016.
Pia
Dkt. Shein alieleza utekelezaji wa sera ya kulipa pensheni kwa wazee, ambapo
amesema hadi mwezi Desemba mwaka 2016, jumla ya shilingi bilioni 4.3 zimetumika
kuwalipa wazee 25,259 waliosajiliwa kiasi cha shilingi 20,000 kila mwezi, zoezi
ambalo litaendelea kutekelezwa.
Katika
hatua nyingine, Dkt Shein alitangaza rasmi kuwa matangazo yote ya TV yatahama
kutoka mfumo wa 'Analogue' na kuhamia mfumo wa 'kidigitali' kuanzia mwezi April
mwaka huu.
No comments