UTAPELI WASTUKIWA KATIKA USAJILI WA GAZETI
Idara
ya Habari (MAELEZO) imebaini nyaraka za kughushi zilizowasilishwa na Mmiliki wa
Kampuni ya FUKANI, Joseph Sheka wakati alipoziwasilisha kwa ajili ya kusajili
gazeti la LETE MAMBO.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa MAELEZO, Dkt.
Hassan Abbasi amesema kuwa mtuhumiwa huyo aliwasilisha nyaraka mbalimbali
akidai kuwa ni za Mamlaka ya Mapato (TRA) ambazo uchunguzi wa awali umebaini
kuwa mihuri na sahihi za baadhi ya maafisa wa Mamlaka hiyo zilizotumiwa ni za
kughushi.
“Ni
vyema jamii ikafahamu kuwa huu siyo wakati wa kujaribu kuishi kwa njia zisizo
halali, kila mwananchi anapaswa kufuata taratibu zinatohitajika pindi anapotaka
kupatiwa huduma katika maeneo mbalimbali ya ofisi za Umma.
Dkt.
Abbasi alitoa rai kwa ofisi mbalimbali za Umma kuwa makini na nyaraka
zinazowasilishwa na wateja wao kwani zinaweza kuwa na malengo mbalimbali ya
kuiingiza Serikali katika matatizo hivyo kuitia hasara.
Mbali
na hayo Dkt abbasi alisisitiza kuwa wale wanaohisi waliwasilisha nyaraka zao na
kuona kwamba zina utata kuja kuzirekebisha na watakaobainika kuwa walighushi
nyaraka hizo sheria itafuata mkondo wake.
Kwa
sasa Idara ya Habari imemkabidhi mtuhumiwa katika Kituo cha Polisi cha Kati
jijini dar es salaam kwa mahojiano zaidi.
No comments