TUNDU LISSU: SABABU HIZI NDIO ZILIPELEKEA KUMCHAGUA LOWASSA KUGOMBEA URAIS
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kiliamua kumchukua aliyekuwa
waziri mkuu, Edward Lowassa, ajiunge na chama hicho baada ya kubaini katika
utafiti maalum uliofanywa na shirika moja kutoka nchi za nje kwamba alikuwa na
uwezo wa kubeba asilimia 18 ya kura zote katika uchaguzi mkuu kuliko mgombea
mwingine wa urais katika uchaguzi mkuu uliopita.
Hayo
yalizungumzwa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, wakati akihojiwa na
Global TV Online ambapo alisema pia Lowassa aliongoza wagombea wote katika
utafiti huo.
“Wazungu
wakatuambia hivi political personalities zote za Tanzania walimfanyia kila
mmoja wao walimfanyia uchunguzi wake, wakatuambia hivi ‘katika wote hao
ukimweka huyu na huyu, huyu bwana mkubwa Lowassa huyu yeye peke yake anatembea
na asilimia 18 ya Tanzania voters,’ aliyekuwa anamfuata alikuwa na asilimia 11
tu.
Kwahiyo Lowassa alikuwa na eighteen percent ya
likeability ya kupendwa na hao Watanzania akienda huku anaenda na asilimia 18
ya ziada, akienda huku anaenda na asilimia 18 za ziada nyingine ongezeeni,”
alisema Lissu.
“Tukasema
hivi, ‘tunataka kushinda uchaguzi eeh tuzungumze na Lowassa’ na Dkt Slaa
akasema tuzungumze na Lowassa tukamwambia ‘Dkt una mawasiliano naye’ akasema
‘sina mawasiliano naye, ila kuna mtu ambaye anaweza akawezesha mawasiliano naye
ni nani? Askofu Gwajima’ tunaelewana, so this how we got Edward Lowassa.”
No comments