MIL. 369 ZIMECHOTWA KUTOKA AKAUNTI YA CUF NA KUINGIZWA AKAUNTI BINAFSI
Katikati
Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi Julias Mtatiro (kushoto) Mbunge viti maalum na
Severine Mwaijage (kulia) Kaimu naibu katibu mkuu na mkurugenzi wa fedha Jaram
Bashange
Baadhi
ya viongozi waandamizi wa chama hicho kutoka kushoto, Shewaji Mketo, Severina
Mwijage, Julias Mtatiro, Joram Bashange, Abdalaha Mtolela, Juma Mkumbi, wakiwa
katika mkutano na wanahabari kuzungumzia kuhusu fedha za chama.
Dar es salaam.
Wakati
mgogoro ndani ya chama cha wananchi CUF ukiwa haujamalizika na suala hilo kuwa
bado lipo mahakamani, leo January 10 2017 Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi,
Julius Mtatiro amekutana na waandishi wa habari na kutoa kueleza kuwa chama
hicho kimeibiwa fedha za ruzuku kiasi cha Tsh Milioni 369.37.
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema leo mhe Mtatiro ameeleza
kuwa fedha hizo zilitoroshwa kutoka hazina ya serikali kuu ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania January 05 2017 na kuingizwa kwenye akaunti iliyofunguliwa katika benk ya NMB yenye jina la
The Civic United Front tawi la temeke ikiwa
na akaunti namba 2072300456.
Alisema mara baada ya fedha hizo kuwekwa katika akaunti hiyo tarehe 5 Jan 2017, siku moja baada ya kuwekwa fedha hizo 6 Jan 2017 mil 60 ilitolewa kama fedha taslim, na kisha kuhamisha kiasi kilichobakia mil 300 kwenda katika akaunti ya mtu binafsi.
Jana 6 Jan 2017 mshukiwa ambaye fedha hizo ziliamishiwa katika akaunti yake ailianza kuzitoa kwa awamu katika matawi mawili ya benk ya NMB, kupitia tawi la magomeni zilitolewa mil 100 na kisha kutolewa katika katika tawi la NMB kariakoo mil 49 na kutokomea nazo kusikojulikana.
kufatia sintofahamu hiyo alisema chama cha wananchi CUF kupitia bodi ya udhamini kinalaani tukio hilo hutoloshwaji wa fedha hizo na kuelezea kusikikishwa zaidi taasisi nyeti za kifedha nazo kushindwa kusimamia utaratibu wa kitendaji wao.
Aidha Mtatilo aliongeza kuwa rejea barua ya msajili wa vyama vya siasa ambayo iliandikwa 1o oct 2016 kuelezea kusitishwa kutoa rudhuku kwa chama hicho kufatia mgogoro uliopo kati ya viongozi wa chama hicho ila cha kushangaza na kuongeza sintofahamu zaidi fedha hizo zimetolewa.
No comments