SHULE ZA ST. FRANSCIS, KILIMANJARO ISLAMIC NA KAIZEREGE KIDEDEA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI
Baraza
la mtihani Tanzania NECTA limetoa matokeo ya mitihani ya upimaji kwa wanafunzi
wa darasa la nne kwa shule zote za msingi nchini pamoja na ule wa kidato cha
pili kwa wanafunzi wa shule za sekondari yanayoonesha ufaulu kuongezeka kwa
1.9%.
Katibu
Mtendaji wa Baraza lza Mitihani nchini Dkt Charles Msonde ndiye aliyetoa
taarifa hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo katika hali isiyo ya kawaida,
shule tisa kati ya kumi zilizofanya vibaya katika mtihani wa kidato cha pili
nchini, zimetoka mkoani Mtwara kama zinavyoonekana hapa
Amesema
ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.9 kutoka 89.12% mwaka 2015 hadi kufikia
91.02% mwaka 2016 ambapo wanafunzi 372,228 wamepata alama zinazowawezesha
kuingia kidato cha tatu huku wanafunzi 36,737 wakishindwa kufikisha alama hizo.
Shule
ya St. Francis Girls ya Mbeya imeongoza katika shule 10 bora kitaifa katika
matokeo ya mtihani wa kidato cha pili mwaka 2016
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja
ya I, II, na III ni 178,115 sawa na asilimia 43.55
Kuhusu
ufaulu wa masomo, amesema, katika masomo ya Civics, History, Geography,
Kiswahili, Phiysics, Chemistry, Chemistry, Biology na Basic Mathematics
umepanda ikilinganishwa na mwaka 2015.
Aidha
ufaulu kwa somo la English Language pekee ndio ambao umeshuka ikilinganishwa na
mwaka 2015.
No comments