Breaking News

KAMUPUNI YA ECONONNECT KUJA NA MFUMO KI-ELECTRONIKI KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA ELIMU NCHINI

Tafiti zilizotolewa na bank kuu ya dunia kupitia delivery indicators imeonyesha kuwa 37% ya waalimu waliokutwa mashuleni hawakuwa madarasani katika muda wa masomo hali inayopelekea kushuka kwa viwango vya elimu nchini

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini dar es salaam Mkurugenzi mtendaji wa ECONNECT Bwana Hashimu Magesa, amesema kitendo cha kukosekana kwa waalimu madarasani katika muda wa masomo kinaashiria kuwa wanafunzi hawapati elimu kwa kiwango kilichokusudiwa na wizara ya husika na mamlaka yake

Alisema pamoja na changamoto hiyo ya waalimu  ambayo pia inachangia  kumekuwepo na wanafunzi hewa pamoja na utoro uliopitiliza  hali inayopelekea kushuka kwa viwango vya elimu kwa kutokujua kusoma na kuandika

Aidha Bwana Magesa kwa kutambua kuwepo kwa changamoto hizo na nyinginezo zinazoikabi sekta ya elimu hapa nchini taasisi ya ECONNECT imeanzisha mfumo wa Kanzidata utakayoisadia serikali kutatua changamoto za kielimu kwa ujumla

Amesema kuwa mfumo huo wa Kanzidata (DATABASE) utasaidia kuwa na takwim u sahihi zinazohusu kujua idadi shule, waalimu, wanafunzi, madarasa, madawati.

 Alisema kupitia mfumo huo wa mawasiliano utatoa urahisi kati ya utawala wa shule na mzazi/mlezi kwa kutoa taarifa kwa haraka juu ya maendeleo ya elimu kwa mwanafunzi kupitia mawasiliano ya simu za kiganjano ambao utagarimu shilingi mia tatu kwa ajili ya kupata huduma zote hizo

Pia bwana Magesa aliongeza kuwa tayali mradi huo umefanyiwa majaribio katika wilaya ya ilala kukusanya taarifa mbalimbali za kielimu kwa kuzihusisha jumla ya shule 152, kupitia takwimu hizo sahihi ambazo tayali kwa sasa zinawapa taarifa hivyo kuokoa fedha ambazo zingetumika kuchapisha taarifa hizo pamoja na taarifa hizo kufika haraka kwa wahusika.


Hata hivyo taasisi ya ECONNECT imetoa wito kwa serikali kutumia mfumo huo kwa majaribio kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kujiridhisha na ufanisi wake, pia taasisi inawataka wadau mbali mbali wa elimu ikiwa ni pamoja na makampuni,  taasisi na watu binafsi kushirikiana kwa pamoja kuwezesha utekelezaji kwa kutumia mfumo kwa lengo la kuboresha elimu kwa manufaa ya taifa.

No comments