MWENYEKITI WA CHADEMA NA WENZAKE 7 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUHARIBU MALI ZENYE THAMANI YA MIL 75.4 NA VITUNGUU
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Karatu mkoani Arusha,
Thomas Darabe na wenzake saba wamepandishwa kizimbani kujibu shitaka la
kuharibu mali ya thamani ya zaidi ya sh milioni 75.4 na vitunguu.
Pamoja
na Darabe, waliopandishwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha/ Arumeru ni
Charles Lameck ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya watumia maji ya ya vijiji
saba vilivyoko katika wilaya ya Karatu na George Pius.
Wengine
ni Baridi John, Christopher Lameck, Florian Tiofil, Daniel Ninida na Lazaro
Emmanuel.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya watumia maji alishitakiwa na mashitaka manne pekee yake ya
thamani ya zaidi ya sh milioni 60 katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha na
Mahakama ya Wilaya ya Arumeru.
Akisomewa
shitaka la kwanza na Mwendesha mashitaka wa serikali, Charles Gakirwa mbele ya
Hakimu Mkazi Patricia Kisinda, alidai kuwa Desemba 28 mwaka huu mtuhumiwa
alifanya uharibifu wa mali aina ya pampu ya maji ya thamani ya sh milioni tatu
na bomba la maji la sh 448,000.
Shitaka
la pili lililosomwa wakili wa serikali Gakirwa mbele ya hakimu mkazi wa wilaya
ya Arusha , Devotha Msofe ilidaiwa kuwa Lameck alifanya uharibifu katika wa
mfumo wa maji katika kijiji cha Quandet Karatu wa thamani ya zaidi ya sh
milioni 1.6.
Mtuhumiwa
alikana mashitaka yote na alipewa dhamana ya mtu mmoja na wadhamini
wakifanikiwa kukidhi vigezo vyote katika mashitaka hayo.
Katika
mashitaka yaliyowahusu washitakiwa wote, akiwemo Darabe pamoja na Lameck
ilidaiwa kuwa wote kwa pamoja walitenda kosa la uharibifu wa mali kwa kuchoma
pampu ya maji ya thamani ya zaidi ya sh milioni tatu na injini ya maji ya
thamani ya sh milioni 12.
Shitaka
la tatu lililokuwa likiwakabili washitakiwa wote ni kuharibu mazao aina ya
vitunguu ya thamani ya zaidi ya sh milioni 49 na pampu mbili za sh milioni
sita.
Washitakiwa
wote walikana mashitaka hayo na dhamana zao zilikuwa wazi na upelelezi wa kesi
hiyo ulikuwa bado haujakamilika na kesi hiyo itatajwa tena januari 16 mwaka
huu.
No comments