MAHAKAMA YAIAMURU SERIKALI KUREKEBISHA KIFUNGU SHERIA YA MTANDAO
Mkurugenzi
wa Mashtaka (DPP) ameondolewa mamlaka ya kutoa adhabu isiyokatiwa rufaa kwa
mshtakiwa anayekiri makosa ya kimtandao.
Uamuzi
huo umetolewa na Mahakama Kuu,umeipa Serikali miezi 12 kukifanyia marekebisho
kifungu cha 50 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao kilichobatilishwa.
Hata
hivyo, mahakama hiyo imehalalisha vifungu vingine vyote vya sheria hiyo,
ambavyo pia vimekuwa vikilalamikiwa na wadau wa matumizi ya mitandao na
teknolojia ya habari.
Uamuzi
huo umetokana na kesi ya kikatiba, iliyofunguliwa na Mtandao wa Watetezi wa
Haki za Binadamu (THRDC), Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC)na mashirika mengine.
Katika
hukumu iliyotolewa na majaji Profesa John Ruhangisa, Winfrida Korosso na Lugano
Mwandambo, Mahakama ilibatilisha Kifungu cha 50 cha sheria hiyo, lakini
ikaridhia vingine kuwa ni halali.
No comments