MHE MASAUN: MARUFUKU KUNUNUA WA SARE ZA JESHI LA ZIMA MOTO NA UHAMIAJI TOKA TAASISI BINAFSI
Naibu
waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Yusuph Masaun amepiga marufuku
ununuzi wa sare za jeshi la zima moto na uhamiaji kwa taasisi binafsi na badala
yake ameagiza sare hizo zizalishwe katika viwanda vya jeshi la magereza nchini.
Mhandisi
Masauni ameyasema hayo baada ya kutembelea kiwanda cha jeshi la magereza
kilichopo Ukonga kinachoendeshwa kwa nguvu kazi ya wafungwa ikiwa ni
ufuatiliaji, utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania la
kulitaka jeshi hilo liwasimamie wafungwa katika uzalishaji wa sare.
No comments