KUTOKA MBEYA: MHE LOWASSA ATAJWA KUSABABISHA DENI LA MILIONI 1
Jina
la waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa limetajwa na mkaazi mmoja wa Mbeya mbele
ya Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makalla kuwa sababu ya deni la shilingi milioni moja
kutokana na mapenzi ya wafuasi wake.
Mkaazi
huyo wa kata ya Ruanda Nzovwe aliyejitambulisha kwa jina la Amos Mwakyambiki
alidai kuwa wafuasi wa Chadema waliharibu paa la nyumba yake walipopanda kwa
lengo la kufuatilia mkutano wa Lowassa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana,
na kwamba chama hicho kilimuahidi kumlipa fidia ya shilingi milioni moja lakini
hadi sasa ahadi hiyo haijatekelezwa.
Alimueleza
mkuu wa mkoa huo kuwa kutokana na uharibifu huo mkubwa uliofanyika, wapangaji
wake waliamua kuhama nyumba yake hivyo kukosa kipato.
“Naomba
Serikali ya Mkoa inisaidie kuzungumza na meya (wa Chadema) ili niweze kulipwa
stahiki zangu kwani sasa sijui hatma yangu. Kuku niliokuwa nauza kwa ajili ya
kupata nauli kwenda ofisi za jiji wamekwisha,” Mkaazi huyo anakaririwa.
Kutokana
na madai hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alimuagiza Mkuu wa Wilaya kufuatilia suala
hilo huku akitahadharisha wananchi kuhusu matumizi ya nyumba zao wakati wa
kampeni.
“Lakini
na nyie wananchi msikubali nyumba zenu zibadilishwe kuwa viwanja vya siasa,”
alisema Makalla.
Akizungumzia
taarifa hizo, Mkuu wa Idara ya Habari ya Chadema, Tumaini Makele alisema kuwa
chama hicho kitafuatilia kuona ni nani aliyetoa ahadi hiyo kwa mwananchi huyo
na ilikuwa katika mazingira gani ili walifanyie kazi ipasavyo.
No comments