KUTOKA MBEYA:MGANGA WA KIENYEJI AUAWA BAADA YA KUWATAPELI WAFANYABIASHARA KUWA WATAPATA UTAJIRI
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la DOTTO MWAIPOPO mkazi wa Kafundo – Ipinda
wilayani Kyela Mbeya ameuawa kwa kuchomwa kisu ubavu wa kulia na BONIPHACE
KISWAGA Mfanyabiashara na Mkazi Chaugingi Mkoani Njombe kwa madai ya kufanya
utapeli.
Taarifa
ya Polisi Mkoa wa Mbeya imesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 11.01.2017
majira ya saa 4 usiku katika Kitongoji cha Ipinda – Chini, Kijiji na Kata ya
Ipinda, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya.
Inadaiwa
kuwa chanzo cha tukio hilo ni kulipiza kisasi baada ya marehemu kuwatapeli
watuhumiwa pesa ambazo kiasi halisi bado hakijafahamika kwa madai kuwa yeye ni
mganga wa kienyeji na atawasaidia kuwa matajiri.
Aidha
katika tukio hilo mtuhumiwa huyo BONIPHACE KISWAGA alijeruhiwa kwa kupigwa na
wananchi na amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela kwa matibabu.
Watuhumiwa wengine wawili ambao walikuwa pamoja na mtuhumiwa aliyekamatwa
walikimbia na msako mkali unaendelea.
No comments