EWURA YATANGAZA BEI MPYA YA MAFUTA ZITAKAZOANZA KUTUMIKA NCHINI KESHO.
MAMLAKA ya Udhibiti huduma za nishati na majini nchini (ewura) imetangaza bei mpya ya mafuta Petrol, dizeli na mafuta ya taa ambayo itaanza kutumika kuanzia tarehe 4 mwezi januari mwaka 2017.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na mkurugenzi mkuu wa EWURA Bwana Felix Ngamlagosi inaonyesha kuwepo
na mabadiliko ya bei kwa mafuta ya aina zote ukilinganisha na toleo la bei la mwaka jana desemba 07. 2016.
Taarifa
hiyo inaonyesha kuwa bei ya rejereja kwa dizeli na mafuta ya taa mwezi januari
2017 itapungua kwa Tsh 66 kwa lita sawa na asilimia 3.68, kwa upande wa petrol bei
imeongezeka kidogo kwa shs 0.10 kwa lita sawa na aslimia 0.01 ukilinganisha na
teleo la bei za mwaka jana.
Kwa
upande wa bei za jumla kwa mafuta ya dizeli na mafuta ya taa zimepungua nazo
kwa Tshs 66 kwa lita sawa na asilimia 3.91 na Tsh 37 kwa lita sawa na asilimia
2.25, kwa upande wa Petroli bei imeongezeka kidogo Tsh 0.01kwa lita sawa na
asilimia 0.01.
Aidha
taarifa hiyo imeongeza kuwa hakutakuwa na mabadiliko ya bei ya mafuta kwa mkoa
wa Tanga hii ni kutokana na kutokwepo na shehena mpya ya mafuta kwenye bandari
ya Tanga tangu mwezi desemba 2016 hivyo kupelekea bei ya mafuta mkoa huo kwa
mwezi januari kubaki kama ilivyokuwa
mwezi wa desemba 2016.
Pia
taarifa hiyo imebainisha kuwa mabadiliko ya bei ya mafuta ya reja reja katika
mkoa wa Dar Es Salaam Petrol 1890, Diseli 1732 wakati mafuta ya taa itakuwa
1700, mabadiloko ya bei za mafuta nchini yanatokana na mabadiliko ya soko la
mafuta duniani.
No comments