Breaking News

UZINDUZI: MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF)

Akikata utepe kwa niaba ya waziri mkuu Mh. Jenista Mhagama, kushoto kwake ni Mh. Antony Mavunde.

Mh. Jenister Mhagama akitoa hotuba kwa niaba ya mgeni rasmi (waziri mkuu) alipokuwa akizindua mfuko wa hifadhin ya jamii jijini Dar Es Salaam.

Naibu waziri wa Antony Mavunde akifafanua jambo katika uzinduzi huo mapema jijini Dar kuhusiana na faida kwa waajili kuwawekea wafanyakazi wao mafao.

Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa huduma ya utoaji wa mafao ya fidia (WCF) bw Masha Mshumba

Mkurugenzi mkuu wa chama cha waajili nchini (ATE) Dr. Mlimka akiongea katika uzindizu huo.


Mwenyekiti wa bodi ya wadahamani wa Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi Emmanuel Humba akizungumzia uzinduzi na uwezeshaji wautoaji wa huduma kwa mfuko huo.

Katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi Dr. Msigwa akiwasilisha salamu na uzoefu wa matatizo wanayopata wafanyakazi yatokanayo na ajali kazini.

Mara baada ya kukata utepe kuashilia uzinduzi wa mfuko huo, kulia ni Mh. Jenista Mhagama, Antony Mavunde nyuma, Abdallah Possi na nyuma ni Emmanuel Humba.

Wageni waalikwa waliohudhulia uzinduzi huo wa moja kati ya mifuko tisa ya hifadhi ya jamii nchini wa WCF Kisenga Hall makumbusho jijini Dar.

Mh. Jenista Mhagama akitoa cheti cha utambulisho bora kwa watoa huduma bora wa huduma za bima INSURANCE TANZANIA LIMITED AA

Kutoka kushoto ni aliyekuwa spika wa bunge Anna Makinda, Mh. Abdallah  Possi, Mh. Mavunde, aliyemwakilisha waziri mkuu, waziri Jenista Mhagama, Emmanuel Humba, Masha Mshomba, M/kiti wa kamati za bunge (jina halikupatikana)

Mwanamuziki wa nyimbo za asili nchini Mrisho Mpoto akitumbuiza katika uzinduzi wa huduma za utoaji wa mafao ya fidia kwa wafanyakazi

Na Frank Wandiba:
Serikali imesema inatambua mchango wa sekta ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini katika kuhakikisha watumishi wanakuwa na maisha bora mbeleni.

Kupitia sheria ya mifuko ya hifadhi za jamii ya mwaka 2015 pamoja na tangazo la serikali namba 212A la tarehe  ambayo imefanyiwa marekebisho mwaka 2015 ambayo inahitaka mifuko ya hifadhi jamii nchini kuondoa mapungufu yaliyokuwepokwenye sheria ya zamani ya fidia ambayo ilikuwa ikilalamikiwa sana kutokana na kutoa malipo kidogo pamoja na ucheleweshwaji wa mifuko hiyo.

Akisoma hotuba kwa niaba ya waziri mkuu  –Waziri wa sera bunge, kazi, vijana, ajira, na wenye ulemavu Jenista Mhagama anasema, “pamoja na uchanga wa sekta ya mifuko ya jamii nchini, mifuko hiyo kufanikiwa mpaka kufikia kuwa na mifuko saba ya hifadhi ya jamii nchini, ambapo imefanikiwa kuwa na wanachama wapatao 2.1 milioni na michango yenye thamani ya shilingi 1.9 trilioni”.

Hata hivyo waziri Mhagama ametoa wito kwa waajiri wote nchini kuboresha mazingira ya kazi yawe salama kwa wafanyakazi pamoja na kulipa michango yao kwa wakati. 

Vilevile katika kuhakikisha zana ya “HAPA KAZI TU” inafanya kazi waziri Mhagama aliongeza kwa kusema “…ni lazima tutambue waotufanyia kazi ni binadamu na hakuna binadamu aijuaye kesho. Hivyo changieni mfuko huu kwa moyo mmoja sio tu kwa sababu ni hitajio la serikali, bali pia kama motisha kwa wafanyakazi”.

Kutokana na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WCF) kuwa mchanga na kujulikana kwa wananchi wengi,waziri ameishauri bodi ya  kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwafikishia ujumbe na matarajio yay a mfuko huu kwa wafanyakazi na waajiri.

Lakini pia ameongeza katika kutekeleza majukumu vizuri, WCF inahitaji madaktari wenye weledi wa kubainisha magonjwa yatokanayo na ajali kazini, hivyo kuweka mpango endelevu wa namna ya kuwaainisha, kuwawezesha na kuwajengea uwezo.



No comments