Breaking News

SHEIKH JALALA: WATANZANIA ENDELEENI KUDUMISHA UMOJA NA UTULIVU, MAELEWANO NA AMANI

Katika  kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa mtume mohammad (S.A.W.W.) itakayofanyiaka tarehe 12 au 17 mfungo wa sita mwaka 571  watanzania wametakiwa kuwa na huruma, kuvumiliana, kusaidiana hili kuenzi matendo aliyosimamia na kufundisha wakati wa uhai wake.

Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam kiongozi mkuu wa waislamu wa dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania, sheikh Hemed Jalala amesema mtume mohammad  (S.A.W.W) alihimiza kwa nguvu zote umoja, utulivu, maelewano na amani.

Alisema Tanzania ya leo hii inayohaja kubwa ya kuenzi ipo haja kubwa kuenzi amani na utulivu, amani ulipo nchini pamoja na mshikamano ili tuendelee kuwa wamoja  bila kuangalia tofauti zetu za kifikra na kimtizamo.

Aidha sheikh JALALA aliongeza kuwa amani ametajwa katika vitabu vyote vya mafundisho ya mwenyezi mungu kwani ndio nguzo za dini zote, amani ndio uhai wa mwanadam yeyote, amani ndio chanzo cha mwanadam kuabudu mungu wake kwa dini zote iwe uislam na hata Ukristo.

Alisema amani itaendelea kuwepo kama tutaendelea kuheshimiana kwa kuheshimu tofauti zetu za dini, mitizamo na kifikra kwani kutokufanya hivyo ndio chanzo cha kutengeneza chuki hivyo watanzania ni lazima waheshimiane katika kila Nyanja hususani katika Dini na mitizamo.

No comments