SERIKALI YA MISRI YAMKAMATA MWANAHABARI WA AL-JAZEERA
Serikali
ya Misri imedhibitisha kwamba inamzuia mwanahabari kutoka shirika la habari la
AlJazeera aliyekamatwa Ijumaa.
Wizara
ya usalama wa ndani inasema mwanahabari huyo, Mahmoud Hussein, atazuiliwa kwa
kipindi cha siku 15 kwa tuhuma za kuchochea maasi na kusambaza habari za uongo.
Television
ya Al Jazeera ambayo imepigwa marufuku kuendesha shughuli zake nchini Misri, imelaani hatua hiyo ya kukamatwa na kwa
mwandishi huyo.
Kulingana
na Aljazeera, mwanahabari huyo raia wa Misri alikuwa nchini humo kwa ajili ya
likizo.
Aljazeera
television katika taarifa yake imesema inahofia usalama wa mwanahabari huyo.
chanzo Bbc
No comments