RAIA 20 WAUAWA KIKATILI MASHARIKI MWA DR CONGO
Takriban
raia 20 wameuawa katika mauaji ya kikatili katika jimbo la Kivu ya Kaskazini
nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kulinga na taarifa zilizotolewa na
maafisa Jumapili.
Vifo
hivi ni vya hivi karibuni katika wimbi la miaka miwili la ghasia katika jimbo
hilo.
Mauji
hayo yametokea katika mji wa Eringeti, uliopo kilomita 55 kaskazini mwa mji
mkuu wa jimbo hilo wa Beni, mji ambao umekuwa ukikumbwa na misururu ya
mashambulio ambayo tayari yamesababisha vifo vya raia 700, kulingana na afisa
katika mkoa huo Amisi Kalonda, ambaye amewalaumu waasi kutoka Uganda kwa
mashambulio ya hivi karibuni.
Bwana
Kalonda amesema kuwa wajumbe wa kundi la waasi la Allied Democratic Forces
(ADF), kundi lenye idadi kubwa ya Waislam wenye itikadi kali kutoka Uganda
ambao wamekuwa kwenye kanda hiyo kwa zaidi ya miongo miwili , walivamia mji huo
Jumamosi mchana.
"ADF
wamevamia tena wau wa Eringeti na maeneo yanayozingira mji huo asubuhi ,"
aliliambia shirika la habari la AFP, kutoka mji mkuu wa Kivu kusini wa Goma.
"Jana,
waliwauwa raia 10. Miili mingine ya watu kumi na miwili ilipatikana Jumapili
katika vijiji vinavyozingira mji ." alisema Bwana Kalonda akiongeza kuwa
waathiriwa waliuliwa kwa visu au panga''
Kwa
miaka miwili iliyopita eneo linalozingira mji wa Beni limekuwa likikimbwa na
mauaji ya kikatili yaliyowauwa mamia ya raia, wengi wao wakichinjwa na
kunyongwa hadi kufa.
Maafisa
wa Kongo wamekuwa wakiwalaumu waasi wa ADF kwa mauaji hayo , lakini ripoti
kadhaa za wataalam zimekuwa zikisema kuwa makundi mengine, yakiwemo ya
wanajeshi wa serikali yalihusika katika baadhi ya mauaji.
Msemaji
wa jeshi la Kongo Mak Hazukay amethibitisha shambulio, akisema wanajeshi
''waliwauwa waasi wa ADF " lakini akaongeza kuwa " idadi ya raia
waliokufa ni kubwa".
Teddy
Kataliki, mkuu wa shirika maarufu la kiraia katika kanda hiyo, pia alisema kuwa
waliouawa ni 22.
Lakini
kasisi wa kikatoliki katika eneo hilo amesema kuwa waliouawa ni watu 27 na
idadi inaweza kuongezeka zaidi " kama miili ya waliouawa itabainika katika
msitu" unaopakana na mji huo.
Wakati
mauaji ya kikatili ya Beni yalipofanyika Oktoba 2014, ADF walijibu haraka
wakishutumu makundi mauaji hayo kutekelezwa na maafisa wa Jamuhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo na MONUSCO---Kikosi cha kulinda amani nchini DRC.
Kwa
zaidi ya miaka miwili sasa, mamlaka za kongo na Umoja wa Mataifa zimeshindwa
kuwalinda raia na ADF limesalia kuwa ndilo kundi linalotawala, huku serikali
ikisisitiza kuhusu uhusiano wa mauaji hayo na vita vya kidini vya Jihad.
Mauaji
haya yanatokea huku mahusiano baina ya jamii ya kimataifa na DRC ukiwa mbaya
kutokana na hatua ya rais Josep Kabila kukataa kuachia mamlaka, licha ya muhula
wake kumalizika taraehe 20 Disemba.
|
No comments