BENKI KUU (BOT) YATOA UFAFANUZI KUHUSU NOTI YA SHILINGI 500
habari
inayoenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba noti ya shilingi mia
tano haitatumika tena baada ya Disemba 31, 2016 sio taarifa ya kweli na ni
uvumi unaopaswa kupuuzwa.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za kibenki BoT, Marcian Kobello ambapo
alifafanua kuwa noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika mzunguko sambamba
na ile sarafu ya shilingi 500 hadi pale noti hiyo itakapotoweka mikononi mwa
wananchi.
Aidha,
Kobello amewataka wananchi kupuuza taarifa zinazoeleza vinginevyo kwani si za
kweli.
Serikali
iliamua kuleta sarafu ya TZS 500 baada ya kuwepo malalamiko kuwa noti ya TZS
500 ambayo ndiyo inazunguka zaidi inachakaa mapema sana.
No comments