SAKATA LA MAITI ZILIZOOKOTWA MTO RUVU, WAZIRI MKUU MAJALIWA ATOA NENO.
Waziri
Mkuu Majaliwa amesema serikali imepokea kwa huzuni kubwa taarifa ya kuokotwa
kwa miili hiyo Desemba 8, mwaka huu na kueleza kuwa matukio kama hayo, likiwemo
la mjasiriamali kuuawa baada ya kutekwa mkoani Tabora, hayavumiliki wala
kukubalika.
Alitoa
maagizo hayo jana katika Baraza la Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W)
lililofanyika kitaifa kijijini Shelui wilayani Iramba mkoani Singida. Waziri
Mkuu Majaliwa alikuwa mgeni rasmi.
Alisema,
“Serikali kwa kushirikiana na Polisi, tena Waziri wa Mambo ya Ndani uko hapa
(akimzungumzia Mwigulu Nchemba aliyekuwepo katika baraza hilo), tutaendelea na
upelelezi ili wahusika wachukuliwe hatua kali.”
Jana akihojiwa katika kituo cha televisheni cha Star TV, Mwigulu alisema uchunguzi umebaini kuwa miili saba iliyookotwa Bagamoyo ni ya wahamiaji haramu.
Jana akihojiwa katika kituo cha televisheni cha Star TV, Mwigulu alisema uchunguzi umebaini kuwa miili saba iliyookotwa Bagamoyo ni ya wahamiaji haramu.
Miili
ya watu sita ilikutwa Desemba 7, mwaka huu kando ya mto Ruvu wilayani Bagamoyo
ndani ya mifuko ya sandarusi na ikiwa imewekwa mawe ili isielee kisha mifuko
hiyo kushonwa kama mzigo wa mazao na kutupwa mtoni.
Mwili
mwingine uliokotwa Desemba 9, eneo hilo hilo na pamoja na kutokuwa katika mfuko
wa sarandusi, ulikuwa umevuliwa shati na kuonekana na majeraha mgongoni na
kwenye ubavu umekatwa na kitu chenye ncha kali.
Mwishoni
mwa wiki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniventure Mushongi alisema miili
yote ilizikwa kwa kuwa ilikuwa vigumu kuwatambua kutokana na kuharibika vibaya
huku kukiwa hakuna kitambulisho chochote kinachoashiria watu hao ni nani na
wametoka wapi na kwamba Polisi inaendelea na upelelezi kubaini waliohusika na
mauaji hayo na atakayebainika sheria itachukua mkondo wake.
Aidha,
Waziri Mkuu alisema serikali ipo macho kukabiliana na tishio lolote la usalama
na vyombo vya usalama vipo tayari muda na wakati wote.
Aliwataka
wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama kutoa taarifa wanapoona kuna hatari
kwani viongozi wa dini na waumini wa dini hizo ndio walinzi wa Taifa.
Alisema
uwepo wa vikundi vya uhalifu kama ‘panya road’ cha jijini Dar es Salaam ni
hatari kwa jamii, kwani vinadhuru na kuvuruga amani na kueleza kuwa ni vijana
na watoto wanaoishi katika jamii, walioko misikitini na makanisani na kutaka
waripotiwe katika vyombo vya usalama ili washughulikiwe.
Alizungumzia
ugaidi na kubambikizwa kesi, na kusema serikali itaendelea kusimamia mtu kupata
haki zake na anayestahili adhabu, kuipata vile vile.
“Ni
heri kuwa na watu 10 waliotoroka mahabusu kuliko mtu mmoja kukaa mahabusu kwa
kesi ya kuonewa,” alisema Majaliwa.
Mwigulu
anena kuhusu miili 7, Saanane
Akizungumza
jana kwa simu kuhusu vifo hivyo vya Bagamoyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba alisema serikali baada ya tukio hilo ilichukua hatua kupitia
vyombo vya usalama na tayari Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali,
Ernest Mangu amemhakikishia wanalifanyia kazi.
“Kama
nilivyosema awali, hatujajua asilimia mia kwa mia kama watu hao waliouawa wana
connection (uhusiano) na wahamiaji haramu waliookotwa wamechoka sana hivi
karibuni (juzi).
“Kuna
wahamiaji 81 waliokotwa hawajitambui, wameishiwa nguvu kabisa, ni eneo hilo
hilo kulikookotwa miili hiyo, tumehisi watu waliowabeba wahamiaji hao
inawezekana wengine walikufa na kwa vile hawana utu, wakawafunga katika viroba
(sarandusi) na kuwatupa, Polisi wanachunguza hili kwa kina,” alieleza Mwigulu.
Aidha,
alisema pia Polisi inachunguza ikiwa miili hiyo ilitupwa kikatili na
wasafirishaji wa binadamu ambao nao hawana utu.
Alipoulizwa
kwa nini wazikwe haraka bila vipimo vya vinasaba, Mwigulu alisema kuwa
alizungumza na IGP na kuelezwa kuwa miili hiyo ilikuwa katika hali mbaya sana,
lakini pia kuzikwa hakuzuii uchunguzi kufanyika kujua chanzo cha vifo hivyo.
Kuhusu
kupotea katika mazingira ya kutatanisha Ofisa wa Ofisi ya Chadema, Makao Makuu
Dar es Salaam, Bernard Saanane Novemba 18, mwaka huu, Mwigulu alisema aliona
taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii na kwa kuwa alikuwa akimfahamu,
alimpigia simu na kubaini simu haipatikani.
“Nilishtuka
kuona hizi habari, binafsi ni rafiki yangu wa karibu, nilipoona hizi habari
nilimpigia na sikumpata, baada ya kuona simpati nilimpigia Mbowe (Freeman-
Mwenyekiti wa Chadema Taifa), lakini simu yake iliita kama vile mtu yupo nje ya
nchi,” alifafanua Mwigulu.
Hata
hivyo, alisema amemuagiza IGP awaagize polisi kumtafuta Saanane na kuhakikisha
ufumbuzi wa kupotea kwake unapatikana na kujulikana alipo.
Juzi,
Mwenyekiti wa Umoja wa Kizazi cha Kuhoji Tanzania (UTG), Malisa Godlisten
akizungumza na waandishi wa habari, aliipa Chadema na taasisi za umma zenye
dhamana ya usalama wa raia saa 72 kuanzia jana kuhakikisha Saanane anapatikana
na kueleza umma chanzo cha vifo vya watu hao saba ambao miili yao ilikutwa
kando ya mto Ruvu, Bagamoyo.
No comments