MCHUNGAJI AWANYWESHA WAUMINI WAKE DAWA YA KUUA BAKTERIA WAPONE MAGONJWA YAO.
Mchungaji
maarufu kwa jina la Rufus Phala kutoka kanisa la AK Spiritual Christian
lililopo Makgodu, Limpopo, Afrika Kusini amewashangaza watu kwa kitendo cha
kuwanywesha Dettol waumini wake ilihali
ina madhara kwa binadamu.
Kwa mujibu wa Daily Sun SA, mchungaji huyo
alifanya kitendo hicho kwenye ibada za kawaida kanisani kwake akiwataka waumini
wenye matatizo na wanaohitaji maombi wanywe Dettol aliyokuwa ameishika mkononi
mwake huku akiwambia watapona shida zao ikiwemo magonjwa.
“Nafahamu kuwa Dettol ni sumu, lakini Mungu
ameniagiza niwape na muitumie. Mimi nilikuwa wa kwanza kuinywa,” – Mchungaji.
Pia alisema kuwa amepokea meseji za
WhatsApp kutoka kwa watu waliokunywa na wamethibitisha kupona. Baada ya kuwepo
kwa taarifa hizo, amehojiwa Daktari kutoka Afrika Kusini, Dr Mabowa Makhomisane,
ambaye amekiri uwa Dettol ina madhara inapotumika tofauti na maelekezo ikiwemo
kuinywa
“Mtu akinywa Dettol na ikafika tumboni,
kimsingi hupunguza mzunguko wa hewa ya Oxygen mwilini. Hali hiyo ikitokea mtu
anaweza kupoteza fahamu na kufariki.
“Na
kama mtu atatapika na bahati mbaya maji maji yakaingia kwenye mapafu yake,
Detto itamsababishia ugonjwa wa Nimonia. Mapafu yatajikunja na mtu atashindwa
kupumua”
Dr Makhomisane amewashauri watu waliokunywa
dawa hizo waende Hospitali kupata vipimo ili kujua madhara waliyopata..
No comments